Habari mpyA

FASS to Strengthen Cooperation with Varsities in the World

By Vincent Mpepo, OUT

Faulty of Arts and Social Sciences of The Open University of Tanzania will continue to cooperate and collaborate with local and foreign higher learning institutions  as a way to ensure it continues with its core responsibilities of teaching, research and service to the community for the benefit of all parties and society as a whole.
 
The statement was made by Dean Faculty of Arts and Social Sciences (FASS) of the Open University of Tanzania, Dr. Dunlop Ochieng when addressing a group of students and lecturers from the Open University of Tanzania and guests from two universities from Norway that are involved in the project sponsored by The Norwegian Agency for Exchange Cooperation (NOREC) held on Friday in Dar salaam.
 
He said his university highly values ​​the collaboration with higher learning institutions from both Tanzania and abroad because the cooperation has benefits including maintaining and developing knowledge and skills in teaching, especially practical training through community service, something that demonstrates the contribution of higher learning institutions to society.
 
“The collaboration between these institutions has helped Tanzanian and Norwegian lecturers and students a platform to practice what they have learnt in the classroom in a real community environment”, said Dr. Ochieng.
 
He said the project is aiming at building up and disseminating knowledge and competencies about children with disabilities, their needs and their rights as described in different national and international conventions. 
 
A Tutorial Assistant in the Sociology and Social Work Department of the Open University of Tanzania, Fauzia Kitenge said while in Norway she learnt many things including the issue of civilization and more how to live with people of different cultures while her call was to tell truth in any situation. 
 
She said despite the great developmental differences between Norway and Tanzania, the fundamentals of humanity to care for others have become the main pillar in both countries as part of valuing humanity.
In addition, she praised the Norwegian medical model which is based on looking at the patient's problem in specialist medical services and expertise in various areas of health, unlike Tanzania where sometimes medical issues are taken as a whole.
 
The representative of students from Himolde University, Karoline Lie their presence in Tanzania and Dar es salaam in particular has taught them many things, including the interpretation and use of force in teaching or giving punishment to children, something that is different in the implementation of teaching policies and laws in the two countries.
 
she said in Norway, there are strict policies and systems that have defined the type of services that every citizen deserves as his/her right in the areas of health, education and social welfare which are different from Tanzania.
 
"With the Norwegian system, each class of pre-primary and primary school students should have a number of students between 20 and 30 and more than one teacher in one session", said Karoline.
 
According to the Head of the Department of Sociology and Social Work of the Open University of Tanzania, Dr. Mariana Makuu, the partnership involves four institutions which are the Open University of Tanzania and Patandi College for Special Needs Education from Tanzania and Molde University College and Western University of Applied Sciences from Norway.
 
 
 
 
 
 

Wafanyakazi CKHT Wakumbushwa Kujaza PEPMIS

Na Vincent Mpepo, CKHT

Wafanayakazi  wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania wamekumbushwa kukamilsha ujazaji wa mfumo wa upimaji na ufuatiliaji wa malengo na shabaha ujulikanao kwa jina la PEPMIS leo 27/01/2024.

Wito huo ulitolewa jana na Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala wa chuo hicho, Francis Badundwa wakati wa mafunzo ya mafunzo ya uingizaji wa malengo ndani ya mfumo wa PEPMISulifanyika jana katika ukumbi wa chuo kikuu huria cha Tanzania kwa ana kwa ana na njia ya mtandao kwa wafanyakazi walio nje ya Dar es salaam.

Alisema ni muhimu kila mfanayakazi ahakikishe amejaza taarifa zake kwenye mfumo huo ili kutoenda kinyume na maagizo ya serikali amabyo inamtaka kufanya hivyo.

Akitoa mafunzo kwa wakuu wa vitivo, wakurugenzi na wakuu wa idara mbalimbali za chuo hicho Ramadhan Kauzen alisema mfumo huo una tofati na OPRAS kwa kuwa una vitu vya ziada ambavyo havikuwepo kwenye OPRAS.

Alisema alisema mfumo wa PEPMIS ni tofauti na OPRAS kwa kuwa unatoa fursa na mawanda mapana kwa mwajiriwa kuweka malengo na shabaha zinazopimika tofauti na mfumo wa OPRAS.

“Kwenye mfumo wa PEPMIS hata sehemu ya majukumu mengine utakayopangiwa na viongozi unaweza kuyaweka na yakapimika”, alisema Kauzen.

Alisisitiza wakuu wa vitivo, wakurugenzi, wakuu wa iadara na viongozi wengine kuwakumbusha wanaowasimamia kujisajikli na kujaza taarifa zao ili wasikose mshahara Mwezi February.

CKHT Kuendeleza Ushirikiano na Taasisi za Elimu Juu Duniani

Na Vincent Mpepo, OUT

Chuo kikuu Huria cha Tanzania kitaendelea kushirikiana na taasisi za elimu ya juu za ndani na nje ya nchi katika kuhakikisha kuwa kinaendeleza majukumu yake ya msingi ya ufundishaji,kufanya utafiti na huduma kwa jamii kwa maslahi ya pande zote na jamii kwa ujumla.

Hayo yalibainishwa na Mkuu wa Kitivo cha Sanaa na Sayansi za Jamii cha chuo hicho Dkt. Dunlop Ochieng wakati akihutubia jopo la wanafunzi na wahadhiri wa Chuo kikuu Huria cha Tanzania na wageni kutoka vyuo vikuu viwili kutoka Norway iliyofanyika jana katika ukumbi wa chuo hicho jijini Dar salaam.

Alisema chuo chake kinathamini sana uhusiano na taasisi za elimu ya juu kutoka nje kwa sababu ushirikiano huo una faida ikiwemo kudumisha na kuendeleza maarifa na ujuzi katika ufundishaji hususani mafunzo kwa vitendo kupitia huduma kwa jamii kitu ambacho kinadhihirisha mchango wa taasisi za elimu ya juu kwa jamii.

‘Watoto wenye mahitaji maalumu na wenye ulemavu wana mahitaji maalumu na maafisa ustawi wa jamii wanafanya kila wazezalo ili kuhakikisha watoto hao wanapata haki zao ambazo wakati mwingine hukiukwa”, alisema Dkt. Ochieng

Alisema ushirikiano uliopo kati ya taasisi hizo umesaidia kuwapa wahadhiri na wanafunzi wa kitanzania na Norway jukwaa la kutekeleza kwa vitendo wakifundisha na kusoma darasani katika mazingira halisi ya jamii.

Mwanafunzi Mtanzania ambaye ni mkufunzi katika idara ya ustawi wa jamii ya Chuo kikuu Huria cha Tanzania, Fauzia Kitenge alisema akiwa nchini Norway alifunza vitu vingi ikiwemo suala la ustaarabu na zaidi namna ya kuishi na watu wa tamaduni za tofauti huku wito wake uikwa ni kueleza au kusimamia ukweli kwa jambo ambalo anaamini ni kweli.

Alisema licha ya utofauti mkubwa wa kimaendeleo kati ya Norway na Tanzania bado misingi ya ubinadamu ya kujali wengine imekuwa nguzo kuu katika nchi zote mbili kama sehemu ya kuthamini ubinadamu.

Aidha alisifu mtindo wa matibabu Norway ambao umejikita katika kuangalia tatizo la mgonjwa katika huduma za kitabibu za kibingwa na ubobevu katika maeneo mbalimbali ya afya tofauti na Tanzania ambapo wakati mwingine masuala ya matibabu huchukuliwa kwa ni kwa ujumlaujumla.

Mwakilishi wa wanafunzi kutoka Chuo Kikuu cha Himolde, Karoline Lie alisema uwepo wao nchini Tanzania wamejifunza vitu vingi ikiwemo tafsiri na matumizi ya nguvu katika ufundishaji au utoaji wa adhabu kwa watoto kitu ambacho ni tofauti katika utekelezaji wa sera na sheria za ufundishaji katika nchi hizo mbili.

Alisema nchini Norway, kuna sera na mifumo thabiti ambayo imeanisha ya aina ya huduma ambazo kila raia anastahili kuzipata kama haki yake katika maeneo ya afya, elimu na huduma za ustawi jamii ambazo ni tofauti na Tanzania.

“Kwa mfumo wa Norway, kila darasa la wanafunzi wa shule za awali na msingi linapaswa kuwa na idadi ya wanafunzi kati ya 20 na 30 na walimu zaidi ya mmoja katika kipindi kimoja”, alisema Karoline.

Kwa mujibu wa Mkuu wa Idara ya sosholojia na ustawi wa jamii ya Chuo kikuu Huria cha Tanzania, Dtk.Mariana Makuu ushirikiano kati ya taasisi hizo unahusisha Chuo Kikuu Huria cha Tanzania na Chuo cha Patandi kwa Tanzania wakati kwa Norway  ni Chuo Kikuu cha Molde na Chuo Kikuu Kishiriki cha Sayansi Shirikishi cha Western.

Serikali Ijenge Mazingira Wezeshi Utekelezaji wa Programu Mbalimbali

Na Vincent Mpepo, OUT

Serikali imetakiwa kuweka mazingira wezeshi kwa taasisi zake ili kuwa namna nzuri ya kutekeleza majukumu kwa taasisi, wakala na mashirika yake ili kuepusha changamoto za mafunzo ya zimatoto katika mambo yake na kufanya vitu vyenye tija kwa maslahi ya umma.

Wito huo umetolewa na wafanyakazi wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania kufutia mafunzo ya Mafunzo ya uingizaji wa malengo ndani ya mfumo wa PEPMIS jana ambayo makataa yake yakiwa ni leo 27/01/2024.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wakati wa mafunzo hayo baadhi ya watumishi wamesema uanzishwaji wa mambo mapya au programu mpya lazima uangalie muda na ratiba za taasisi pamoja na mafunzo ili kufanya utekelezaji uwe mwepesi kwa watumishi.

WAZIRI AWESO NA UDOM KUHUSU MAJI

Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) ameitaka Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA) kuweka mpango mkakati wa dharura wa kuhakikisha upatikanaji wa huduma ya majisafi katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) inapatikana haraka kwa uhakika na ubora.

Mhe. Aweso amesema hayo leo Januari 23,2024 akiwa katika ziara ya kikazi jijini Dodoma katika Chuo Kikuu cha UDOM na chanzo cha maji cha Iyumbu kufuatilia hali ya upatikanaji wa maji chuoni hapo, na ameihakikishia jumuiya ya chuo hicho na wanachuo kuwa hali ya huduma ya maji itaimarika na kwamba kazi ya serikali ni kuwapatia wananchi wote huduma ya majisafi.

Mhe. Aweso amemtaka Mkurugenzi Mtendaji wa DUWASA, Mhandisi Aron Joseph kuhakikisha anaweka mtandao wa maji unaojitegemea ili kutoa huduma UDOM kutoka chanzo cha maji cha Nzuguni, ambapo Wizara ya Maji itawezesha utekelezaji wake.

Aidha, ameitaka DUWASA kuongeza upatikanaji wa maji chuoni hapo kutokana na dharura iliyopo.

Mhe. Aweso katika hatua nyingine ameagiza kuendelea kufanyika utafiti wa kina katika maeneo ya Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) ili kutambua uwepo wa maji chini ya ardhi.

Kwa upande wake, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Prof. Lughano Kusiluka amesema bado UDOM ina uhitaji mkubwa wa majisafi upatao lita 2,296,000 zinazohitajika kuweza kuhudumia wanachuo wapatao elfu 33, ambapo kwa sasa chuo hicho kinapata lita 1,172,000 kutoka DUWASA sawa na asilimia 51 kutoka vyanzo vya Mzakwe na Iyumbu.

Waajiri Sekta ya Umma, Binafsi Walalamikiwauhusa na rasilimali fedha waajiriwa wao ili wajiendeleze kitaaluma.

Lawama hizo zilitolewa na wahitimu wa wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania Kituo cha Mkoa wa Arusha wakati wa mahafali ndogo kwa ngazi ya Mkoa iliyofanyika katika kituo cha mkoa cha Arusha mwishoni mwa wiki huku wakiiomba serikali kuwakumbusha waajiri katika sekta hizo kuwapa stahiki hizo.

Mhitimu wa Shahada ya Umahiri ya Ukutubi na Usimamizi wa Habari, Rafiki Kilonzo alisema baadhi ya waajiri huweka vikwazo mbalimbali ikiwemo kuwacheleweshea ada na kuwanyima muda wa kujiendeleza kielimu.

Aidha alizungumzia changamoto zinakikabili Kituo hicho cha Mkoa ikiwemo ufinyu  wa eneo ambao hautoi mazingira wezeshi kujisomea.

“Eneo lililpo kwa sasa ni dogo na halitoshi kukidhi mahitaji yetu ya kuwa na mazingira mazuri ya kujisomea”, alisema Kilonzo.

Mkuu wa wilaya ya Arusha, Felician Mtehengerwa alisema serikali itaendelea kujenga mazingira wezeshi ili taasisi za elimu ya juu ziendelee kufanya kazi zake kwa ufanisi.

Aidha, alimtaka Mkurugenzi wa Kituo cha Arusha, Dkt.Nangware Msofe kufanya mawasiliano na ofisi yake ili wapewe eneo kwa ajli ya kuendeleza chuo hicho.

“Kwa sasa jiji la Arusha tunagawa maeneo kwa taasisi mbalimbali, hatuwezi kukosa eneo kwa ajili ya chuo chenu”, alisema Mtehengerwa.

Zaidi ya wahitimu 3980 walihitimu katika mahafali ya 42 ya Chuo hicho idadi ambayo inatajwa kuwa kubwa na chachu ya kuongeza rasilimali watu katika sekta ya umma na binafsi huku zaidi ya wahitimu 260 wanatokea Arusha.

Employers Public, Private Sectors Criticized

By Vincent Mpepo, OUT

Employers in the public and private sectors in the country have been balmed for not giving permission and financial support to their employees to develop themselves professionally.

The accusations were made by the graduates of the Open University of Tanzania in Arusha Regional Center during the min graduation held in Arusha over the weekend while the main topic was asking the government to remind employers to act responsibly.

A graduate of Master’s Degree in Library and Information Management, Rafiki Kilonzo said some employers impose various restrictions including denying them time to develop themselves educationally something which is not right.

In addition, she spoke about the challenges facing the Regional Center, including the narrowness of the area which does not provide an enabling environment for self-study.

“The current area is small and not enough to meet our needs to have a good environment to study”, said Kilonzo.

Arusha District Commissioner, Felician Mtehengerwa said the government will continue to create an enabling environment so that higher education institutions can continue to do their work effectively.

Additionally, he asked the Director of the Arusha Center, Dr. Nangware Msofe to communicate with his office so that they can be given an area in order to develop the University.

“Currently in the city of Arusha we are allocating areas to various institutions, we cannot miss an area for your college”, said Mtehengerwa.

More than 3980 graduates graduated in the 42nd graduation held last year and a number is said to be large and a catalyst for increasing human resources in the public and private sectors, while more than 260 graduates comes from Arusha.

Habari za zilizobamba

Information center summary

matangazo

Blog at WordPress.com.