• Na Grace Mwakalinga, RUKWA

    MKUU wa Wilaya ya Kalambo Mkoani Rukwa, Lazaro Komba, ameviagiza vyombo vya ulinzi na usalama  wilayani humo kuhakikisha vinadhibiti mienendo inayolenga kuhatarisha ustawi wa watoto  wakiwemo wenye ualbino katika jamii.

    Komba alitoa kauli hiyo hivi karibuni wakati wa kujadili masuala ya  kuimarisha ulinzi na usalama wa watoto ili kulinda haki ya msingi ya kuishi.

    “Imani potofu zimesababisha watoto  wenye ulemavu hususani wenye ualbino kufanyiwa ukatili kama vile kuuawa na kunyofolewa baadhi ya viongo  kwenye miili yao”, alisema Komba.

    Kutokana na suala hilo kuripotiwa katika baadhi ya maeneo nchini, Komba alisema tayari wilaya ya Kalambo imeanza kutekeleza maagizo ya Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa  kwa kuweka mikakati kuanzia ngazi ya kitongoji kwa kutumia vyombo vya ulinzi na usalama kuthibiti vitendo hivyo.

    “Ulinzi na usalama kwa watoto wenye mahitaji maalum ni jukumu la kila mmoja wetu, tushiriki kuhakikisha wanalindwa dhidhi ya ubaguzi, unyanyasaji na ukatili wa aina zote ikiwemo mauaji ya watoto wenye ualbino,” alisema Komba.

    Aliongeza kuwa tayari baadhi ya wadau wanaendelea kutekeleza jukumu la ulinzi na usalama wa watoto wenye mahitaji maalum wakiwemo wenye ualbino ambao ni Child Support Tanzania (CST), kukemea na kupinga ukatili na mauaji dhidi ya watu wenye Ualbino yaliyoripotiwa hivi karibuni likidai vitendo hivyo vinajenga hofu na kutishia usalama kwa makundi hayo.

    Mratibu wa shirika la Child Support Tanzania (CST), Nemes Temba alisema wananchi wanapaswa kuachana na imani potofu dhidi ya watu wenye ualbino kwa kuwa kuendeleza imani hizo ni kwenda kinyume na maagizo ya vitabu vitakatifu, katiba ya nchi na mikataba mbalimbali ya kitaifa na kimataifa ambayo inasisizita haki ya kuishi kwa kila mtu bila kujali hali aliyonayo.

    Alisema jukumu la jamii ni kufungua fursa za kielimu  na kuweka mazingira rafiki kwa watoto wenye mahitaji maalum ili kuwasaidia kutimiza ndoto zao.

    “Tulikuwa na maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika hapa mkoani Rukwa ambayo ilikuwa mahsusi kujadili na kuangalia masuala ya kuyatekeleza ili kuhakikisha ulinzi na usalama kwa watoto wenye mahitaji maalum.

    Alisema miongoni mwa miradi wanayotekeleza ni kuhakikisha watoto wenye ulemavu wanapelekwa shule kuanza masomo, uboreshwaji wa miundombinu ya shule  jumuishi zilizopo mikoa ya Mbeya, Songwe, Rukwa na Katavi pamoja na utoaji wa vifaa vya kufundishia na kujifunzia kulingana na ulemavu wa kila mmoja.

    “Kauli mbiu ya mtoto wa Afrika  mwaka huu inazungumzia Elimu Jumuishi kwa watoto izingatie  maadili na maarifa na stadi za maisha inahimiza jamii kutoa elimu yenye usawa kwa watoto wote, wenye ulemavu na wasio na ulemavu,” alisema Temba.

  • Na Grace Mwakalinga, Dodoma

    Wadau wa sekta ya Sanaa wamekutana jijini Dodoma kujadili vikwazo wanavyokabiliana navyo wakati wa kutekeleza majukumu yao.

    Kikao hicho kimefanyika leo jijini humo kimewahusisha wadau ikiwemo Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Baraza la Kiswahili Tanzania (BAKITA) na Taasisi ya Hakimiliki (COSOTA) ili kupata suluhu ya masuala yanayohusu haki na maslahi  ya wasanii Tanzania.

    Agness Kahamba, msanii wa maigizo nchini amesema wanapitia changamoto nyingi wakati wa kutekeleza majukumu yao na kwamba vinapoandaliwa vikao kama hivyo vinatoa fursa kueleza wanayoyapitia ili kupata suluhu kwa wadau wao.

    “Tunatamani kufanya Sanaa yetu kibishara kwa kuuza bidhaa tunazozizalisha ndani na nje ya nchi  lakini  changamoto ni maslahi duni na kukosa mitaji ya kuandaa kazi bora zenye ushindani. Tunaimani Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kupitia ziara alizozifanya mataifa mbalimbali zinaendelea kutangaza sanaa zetu,” amesema Agness.

    Mkuu wa Idara ya Sheria wa Kituo cha Kutetea Haki za Wasanii Tanzania (TARO), Ally Ramadhan, amesema wameendesha vikao mbalimbali kuhusu wasanii na kupokea mapendekezo yao.

    Amesema baada ya mapendekezo hayo watayachakata na hapo baadae watayapeleka bungeni kwa ajili kufanyiwa maboresho na kutungwa kwa sheria zitakazoendelea kuwalinda wasanii nchini.

    Kwa upande wake wakili wa Baraza la Sanaa la Taifa,    Joseph Ndosi, amesema wao kama    walezi wa sekta ya Sanaa wataendelea kuwashauri wasanii namna bora ya kuzalisha kazi zenye ushindani ili kufikia malengo waliyokusudia.

  • Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Thomas Apson akiongea na waandishi wa habari katika maadhimisho ya siku ya uhuru wa habari yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano uliopo kwenye jengo la ofisi za madini Mkoa wa Singida Mei 15, 2024

    Na Sylvester Richard-Singida

    Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Thomas  Apson amesema serikali itaendelea kushirikiana na waandishi wa habari wa Mkoa wa Singida ili kulinda na kukuza demokrasia nchini ikiwa ni namna ya kuhakikksha kuwa  wananchi watapata taarifa kuhusu nini serikali yao ili kuharakisha maendeleo kupitia vyombo vya habari.

    Apson  aliyasema hayo Mei 15, 2024 wakati wa maadhimisho ya siku ya uhuru wa habari kwa Mkoa wa Singida yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano jengo la ofisi za madini Mkoani hapo.

    Alisema Serikali inatambua mchango mkubwa wa wanahabari katika kukuza uchumi wa Taifa na wa Mtu mmoja mmoja na ndiyo maana imetoa uhuru kwa wanahabari kufanya kazi zao kwa kuzingatia maadili ya kazi za pamoja na sheria zilizowekwa.

    Alisema  uhuru huo wa vyombo vya habari umeenda sambamba na uhuru wa kufanyika kwa mikutano ya hadhara, vikao na maandamano kwa vyama vyote vya siasa ambapo wanahabari wamekuwa wakiandika habari juu ya mikutano hiyo yenye lengo la kuikosoa na kuishauri serikali iliyopo madarakani.

    Mwenyekiti wa Klabu ya wanahabari Mkoa wa Singida (SINGPRESS, Elisante John akitoa taarifa ya Klabu kwa Mkuu wa Wilaya ya Ikungi katika maadhimisho ya siku ya uhuru wa habari Mkoa wa Singida.

    Mwenyekiti wa Klabu ya wanahabari Mkoa wa Singida ( SINGPRESS) Elisante John alisema Klabu hiyo ilianzishwa Julai 16, 2023 kwa lengo la kuwaunganisha wanahabri  wa Mkao  huo ili kufanya kazi chini ya mwamvuli mmoja unaoongozwa na katiba ya Klabu.

    Alisema Klabu hiyo ina malengo ya kukuza demokrasia katika jamii kupitia fursa sawa zinazotolewa na vyombo vya habari kwa kutoa taarifa sahihi katika masuala ya elimu kwa makundi mbalimbali ikiwemo wanawake, watoto, vijana, wazee na wenye ulemavu.

    Kwa upande wake, Mkurugenzi  Mtendaji  wa Shirika la Research and Development organization (ReDO),Hudson Kazonta aliwataka waandishi wa habari kuandika habari mazingira ili kutoa elimu ya utunzaji mazingira kwa Wananchi na utambuzi wa mabadiliko ya tabia nchi.

    Maadhimisho hayo yalifanyika kimkoa baada ya kufanyika kimataifa Mei 3, 2024 Jijini Accra Ghana na kitaifa jijini Dodoma yalibebwa na kauli mbiu isemayo ” Uandishi wa Habari na Changamoto za Mabadiliko ya Tabia Nchi” na yamefanyika mara 31 tangu kuanziahwa kwake mwaka 1993.

  • Na Sylvester Richard- Singida

    Katibu Tawala Mkoa wa Singida Dkt. Fatma Mganga akihutubia wananchi wa Mkoa wa Singida waliofika katika ukumbi wa RC Mission Manispaa ya Singida kwenye hafla ya kumuaga aliyekuwa Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo DCP Stella A. Mutabihirwa aliyehamishiwa Makao Makuu ya Polisi na kumkaribisha Kamanda SACP Amon Daudi Kakwale.

    Katibu Tawala Mkoa wa Singida Dkt. Fatma Mganga amewataka askari wa Mkoa wa Singida kukataa rushwa kila mahali wanapokutana na watu wasio waaaminifu wanaotaka kuwahadaa na  kuwapa rushwa ili wafanye udanganyifu wa kesi mbalimbali.

    Mganga amesema hayo Mei 3, 2024 katika hotuba yake aliyoitoa kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Singida aliyealikwa kuwa Mgeni Rasmi kwenye hafla ya kumuaga aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida DCP Stella Alchard Mutabihirwa iliyofanyika kwenye ukumbi wa RC Mission Manispaa ya Singida.

    Aidha, Dkt. Mganga amewasisitiza askari kutosheka na mishahara yao na kuepuka kujiingiza kwenye vitendo vya rushwa ambavyo vinarudisha nyuma maendeleo ya nchi na ya mtu mmoja mmoja.

    Kwa upande mwingine, amewaomba viongozi wa dini kuendelea kuiombea Nchi ili iendelee kuwa na amani na wananchi wake waishi katika maadili.

    Akiwaaga askari wa Mkoa wa Singida, DCP Mutabihirwa amewashukuru askari na wananchi wa Mkoa wa Singida kwa ushirikiano waliompa katika kipindi alichokuwa Mkoani humo akiwa na cheo kidogo hadi alipoondoka na cheo cha Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) huku akiuacha Mkoa ukiwa shwari.

    DCP Stella A. Mutabihirwa akiwaaga askari na wananchi wa Mkoa wa Singida kwenye hafla iliyofanyika kwenye ukumbi wa RC Mission baada ya kuhamishiwa Makao Makuu ya Jeshi la Polisi Dodoma.

    Naye Kamanda wa Polisi wa sasa wa Mkoa wa Singida SACP Amon Daudi Kakwale ambaye pia amepokelewa rasmi katika hafla hiyo ameahidi kuendeleza mazuri aliyoyafanya DCP Mutabihirwa wakati akiwa Kamanda wa Mkoa huo.

    Hata hivyo, Kakwale amewaomba askari na wananchi wa Mkoa wa Singida kumpa ushirikiano katika kubaini, kupambana na uhalifu ili Mkoa wa Singida uendelee kuwa shwari.

  • Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida SACP Amon Daudi Kakwale akiongea na makundi ya watu katika ukumbi wa mikutano uliopo kwenye jengo la Makao Makuu ya Jeshi la Polisi Mkoa wa Singida.

    Na Sylvester Richard- Singida

    Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida SACP Amon Daud Kakwale amewataka viongozi wa Serikali za Mitaa kuwatumia Polisi Kata katika kuimarisha ulinzi na usalama wa maeneo yao kwa kutoa taarifa za wahalifu kwa usahihi na kwa wakati.

    Alisema hayo Mei 3, 2024 wakati akizungumza na makundi mbalimbali ya watu wa Manispaa ya Singida wakiwemo viongozi wa Serikali za Mitaa, viongozi wa vyama vya siasa, viongozi wa madhehebu ya dini, wazee wa kimila na wamiliki wa makampuni ya ulinzi binafsi kwenye kikao  kilichofanyika ukumbi wa mikutano uliopo katika jengo la Makao Makuu ya Jeshi la Polisi Mkoa wa Singida.

    Aidha aliwataka viongozi hao kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa sahihi za viashiria vya changamoto za kiusalama ili zifanyiwe kazi.

    Kikao hicho ambacho pia Kamanda Kakwale amekitumia kujitambulisha, kilikuwa huru na wazi ambapo wajumbe walipata nafasi ya kutoa kero na kuchangia hoja mbalimbali zilizolenga kuimarisha ulinzi na usalama wa Mkoa wa Singida.

    Kwa upande wake, Mstahiki  Meya wa Manispaa ya Singida Yagi Kiaratu ambaye pia alihudhuria kikao hicho,  alilipongeza Jeshi la Polisi kwa kupeleka huduma ya Polisi kwenye Kata na kusema kuwa Polisi kata wamekuwa msaada mkubwa kwa jamii kwakuwa uhalifu umekuwa ukipungua siku hadi siku.

    Mstahiki Meya wa Manispaa ya Singida Yagi Kiaratu akichangia hoja katika kikao cha Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida na makundi mbalimbali ya wakazi  wa Manispaa ya Singida.

    Aaliliomba Jeshi la Polisi lishirikiane na Mshauri wa Mgambo Wilaya katika kuwafundisha vijana wenye sifa juu ya ulinzi shirikishi ili vijana wafanye kazi ya ulinzi kwa uelewa zaidi.

    Katibu wa CHADEMA Jimbo la Singida Mjini, Mtta Anselemi  Adrian akichangia hoja kuhusu ulinzi na usalama.

  • Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe. Halima Dendego akiongea na watumishi wa umma Mkoa wa Singida katika kituo cha mabasi Ikungi kwenye maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani.

    Na Sylvester Richard-Singida

    Mkuu wa Mkoa wa Singida Halima Dendego amewataka watumishi wa umma Mkoa wa Singida kuisikiliza na kuielewa hotuba Mh.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassani iliyowasilishwa kwa niaba yake na Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango kwenye maadhimisho ya Mei Mosi 2024 yaliyofanyika kitaifa Mkoani Arusha.

    Dendego amebainisha hayo jana Mei 1, 2024 wakati akizungumza na watumishi wa umma kwenye maadhimisho ya siku ya wafanyakazi Duniani  yaliyofanyika  kimkoa kwenye kituo cha mabasi Wilayani Ikungi.

    Baadhi ya mambo yaliyoahidiwa na serikali kwa wafanyakazi kupitia hotuba hiyo ni pamoja na kuhuisha viwango vya mishahara kwa kuzingatia uwezo wa kiuchumi na kibajeti pamoja na ujuzi na utendaji wa waajiriwa misingi ambayo imetajwa kuwa ni muhimu ili kuepuka mfumuko wa bei na uhimilivu wa deni la taifa na athari nyiningine za kichumi.

    Aidha, Dendego amewakumbusha watumishi kufanya kazi kwa kuzingatia kanuni  na maadili ya kazi ili kuongeza ufanisi katika kazi. Maadhimisho hayo yalibebwa na kaulimbiu isemayo “Nyongeza ya mshahara ni msingi wa mafao bora na kinga dhidi ya hali ngumu ya maisha” na yaliambatana na utoaji wa zawadi ambapo Dendegu alikabidhi zawadi mbalimba kwa wafanyakazi wa Mkoa wa Singida waliofanya vizuri mwaka 2024.

  • Na Vincent Mpepo, OUT

    Imeelezwa kuwa ujio wa teknolojia mpya unapaswa kuchukuliwa kwa mapokeo chanya ili isadie katika mifumo ya ujifunzaji na usomaji katika ngazi zote za elimu badala ya kuweka vizuizi vingi katika utekelezaji wake.

    Hayo yamebainishwa na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, Profesa Elifas Bisanda wakati wa kusaini makubaliano kati ya Chuo Kikuu Huriacha Tanzania na Chuo Kikuu cha Masafa cha Sayansi Tumizi  cha Uswisi yaliyofanyika hivi karibuni katika ukumbi wa chuo hicho Kinondoni jijini Dar es salaam.

     Akizungumzia masharti na vizuizi vya wanafunzi kutumia teknolojia mpya ikiwemo ya AI na ChatGPT katika ujifunzaji alisema wakati umefika kwa walimu na wahadhiri kuuliza maswali ambayo yatasaidia kuwashughulisha wanafunzi badala ya yale yaliyozoeleka.

    “Muulize maswali yatakayomfanya atafute majibu nje ya AI na ChatGPT, siyo yale ya kujadili au kutoa fasili ya dhana fulani”, alisema Profesa Bisanda.

    Profesa Bisanda alisema kwa sasa ufundishaji na ujifunzaji katika elimu ngazi zote unapaswa kuhusisha teknolojia ili kuwafikia wahitaji wengi na kwa muda mfupi lakini pia kurahisisha mchakato wa elimu tofauti ilivyokuwa hapo awali.

    “Watu wanaanza kuwa na woga na AI na ChatGPT  sawa na kwa waliosoma zamani kidogo ambapo ilikuwa ni kosa la jinai kutumia kikokotoo au kompyuta lakini kwa sasa vimekuwa vitu vya kawaida”, alisema Profesa Bisanda.

    Alisema mazingira ya kazi yanapaswa kuendana na mazingira ya kusoma yanayotawaliwa na simu janja na kompyuta badala yake tuwafundishe wanafunzi ili wapate maarifa, ujuzi na stadi za kazi au taaluma wanazosomea.

    Afisa Mwandamizi, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt.Evaristo Mtitu alipongeza jitihanda za chuo hicho katika uwekezaji kwenye Tehama na teknolojia nyingine wezeshi katika masuala ya ujifunzaji na ufundishaji.

    “Vyuo vikuu na taasisi za elimu ya juu zinapoingia kwenye mkataba wa maelewano ya kushirikiana kwenye maeneo ya makubaliano inasaidia  kubadilishana uzoefu kwenye maeneo ya ushirikiano”, alisema Dkt.Mtitu.

    Alisema vyuo vyote vinatakiwa kuwekeza kwenye matumizi ya teknolojia ili kurahisha mchakato wa kujifunza na kufundishia.

    Aliongeza kuwa wizara inaamini kuwa teknolojia zinasaidia kuwa na rasimali watu inayoweza kutumika kuwafikia walengwa wengi kwa muda mfupi mfano walimu wa sayansi.

    “Teknolojia ikitumika vizuri inatoa nafasi kwa mwanafunzi kushiriki vizuri kwenye kipengele cha ujifunzaji mwenyewe”, alisema Dtk.Mtitu. 

  • Mkuu wa Mkoa wa Singida Halima Dendego akiongea na wananchi wa Mkoa wa Singida katika maadhimisho ya miaka 60 ya kuzaliwa kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Mji Mdogo wa Kiomboi, Wilaya ya Iramba, Mkoani Singida.

    Na Sylvester Richard, Singida

    Watanzania wamekumbushwa kuuenzi muungano wa Tanganyika na Zanzibar kwa kufanya kazi kwa maarifa na juhudi ili kujiletea maendeleo.

    Wito huo umetolewa na  Mkuu wa Mkoa wa Singida, Halima Dendego wakati wa maadhimisho ya miaka 60 ya muungano kati ya Zanzibar na Tanganyika yaliyofanyika leo maeneo ya kituo cha mabasi kilichopo katika Mji Mdogo wa Kiomboi, Wilaya ya Iramba Mkoani Singida huku wito wake ukiwa ni kufanya kazi zaidi.

    Dendego aliwapongeza wasanii waliosherehesha katika maadhimisho hayo zikiwemo kwaya, ngoma za asili, mziki wa kizazi kipya na wachoraji na kuwataka kudumisha utamadini, mila na desturi za mtanzania.

    “Sanaa ni furaha, ni afya, ni kazi na ni ajira”, alisema Dendego.

    Aidha, katika maadhimisho hayo Dendego alipokea zawadi zilizoandaliwa na baadhi ya wasanii huku pia yeye akikabidhi zawadi kwa makundi mbalimbali kama zilivyoandaliwa na kamati ya maadhimisho hayo.

    Katibu Tawala Mkoa wa Singida Dkt. Fatma Mganga ambaye alihudhuria maadhimisho hayo aliwaasa wananchi wa mkoa huo kuendeleza mshikamono walionao katika nyanja zote ili kujijenga na kukua kiuchumi kama muungano unavyotaka kwa maendeleo yao na mkoa kwa ujumla.

    Katibu Tawala Mkoa wa Singida Dkt. Fatma Mganga akiongea na
    wananchi katika maadhimisho ya miaka 60 ya kuzaliwa kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yaliyofanyika katika Mji Mdogo wa Kiomboi, Wilaya ya Iramba Mkoani Singida.

    Maadhimisho hayo yamefanyika kitaifa na kwa ngazi za mikoa na wilaya kwa namna mbalimbali huku yakiongozwa na kauli mbiu isemayo,”Tumeshikamana  na tumeimarika, kwa maendeleo ya taifa letu”.

  • By Vincent Mpepo, OUT

    The Vice Chancellor of the Open University of Tanzania, Professor Elifas Bisanda exchanging partnership agreements with Professor Egon Werlen of Swiss Distance University of Applied Sciences during the MoU signing held today in Kinondoni, Dar es Salaam (Photo by Vincent Mpepo).

    The Open University of Tanzania and Swiss Distance University of Applied Sciences have signed a five year Memorandum of Understanding which will help the two to collaborate in various academic activities for the betterment of two universities and countries at large.

    Speaking during the official signing of the MoU between the two universities, the Vice Chancellor of the Open University of Tanzania, Professor Elifas Bisanda said the collaboration will involve a number of areas of agreement which involves students and lectures exchange, fellowships, scholarship and collaborative research.

    He welcomed and thanked the Swiss Distance University of Applied Sciences for having an interest to collaborate with the Open University of Tanzania and assured that his university will keep on cherishing the good things for the benefit of two universities.

    Dean Faculty of Arts and Social Sciences, Dr.Dunlop Ochieng said the collaboration has been a very fruitful because it has brought a number of benefits for both universities.

    “FASS is very grateful and proud for this collaboration that started with the faculty and has now extended to university wide”, said Dr.Ochieng.

    He said his faculty is committed to encouraging faculty members to actively participate in future research stemming from the present study under the auspices of the OUT UNESCO Chair on curriculum development.

    A researcher from the Open University of Tanzania, Dr.Christopher Awinia shared the findings of a research which was part and parcel of the collaboration between two universities where it has been found that technological challenges hamper learning and teaching environment in Tanzania.

    He identified some of the challenges as stemming from internet cost and unreliable internet something which makes learning and teaching in Tanzania and most of African countries to face some difficulties hence legging behind in education.

    Senior Education Officer from the Ministry of Education, Science, and Technology, Dr. Evaristo Mtitu addressing the public during the signing ceremony between the Open University of Tanzania and Swiss Distance University of Applied Sciences held today in Kinondoni, Dar es Salaam (Photo by Vincent Mpepo).

  • Na Mwandishi wetu, Dar es salaam

    Kanisa la DPA la jijini Dar es salaam litafanya maadhimisho ya miaka minne tangu kuanzishwa kwake kama sehemu tathimini na shukrani kwa Mungu.

    Hayo yamebainishwa na Mchungaji muasisi wa kanisa hilo, Hanington Kabuta wakati wa mahojiano na mwandishi wetu huku akitanabaisha kuwa madhabahu hiyo ya DPA imekuwa baraka kwa mtu mojamoja na jamii kwa ujumla na kwamba Mungu amewatendea mengi.

    “Mwezi huu wa nne mwaka 2024 kanisa letu la DPA limefikisha miaka 4 tangu lianzishwe hapa Goba, Tegeta A, Mtaa wa Msabila”, alisema Mchungaji Kabuta.

    Alisema uongozi wa kanisa hilo umeamua kufanya maadhimisho ndani ya wiki hii, ambapo kilele chake ni Jumapili jioni.

    Tuna maombi ya mfungo wiki hii pamoja na Semina ya Historia ya Kanisa Kiulimwengu, Afrika, Tanzania, na Hatimaye DPA, alibanisha Mchungaji Kabuta.

    Aliongeza kuwa semina ni Jumatano tarehe 24 hadi Junapili tarehe 28/04/2024 na  Muda ni kuanzia saa 10:00 Jioni hadi 12:30 Jioni kwa siku hizo tano huku agenda kuu ni ‘Fundisho la Kanisa, Maombi na Maombezi.

    Aliwataka watu wote wenye mapenzi mema kuhudhuria na kuwaalika wengine huku akiwakumbusha kushirikisha taarifa hii kwenye mitandao ya kijamii ili wengi waokolewe.