Na Vincent Mpepo, CKHT

Wafanyakazi  wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania wamekumbushwa kukamilsha ujazaji wa mfumo wa upimaji na ufuatiliaji wa malengo na shabaha ujulikanao kwa jina la PEPMIS leo 27/01/2024.

Wito huo ulitolewa jana na Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala wa chuo hicho, Francis Badundwa wakati wa mafunzo ya mafunzo ya uingizaji wa malengo ndani ya mfumo wa PEPMISulifanyika jana katika ukumbi wa chuo kikuu huria cha Tanzania kwa ana kwa ana na njia ya mtandao kwa wafanyakazi walio nje ya Dar es salaam.

Alisema ni muhimu kila mfanayakazi ahakikishe amejaza taarifa zake kwenye mfumo huo ili kutoenda kinyume na maagizo ya serikali amabyo inamtaka kufanya hivyo.

Akitoa mafunzo kwa wakuu wa vitivo, wakurugenzi na wakuu wa idara mbalimbali za chuo hicho Ramadhan Kauzen alisema mfumo huo una tofati na OPRAS kwa kuwa una vitu vya ziada ambavyo havikuwepo kwenye OPRAS.

Alisema alisema mfumo wa PEPMIS ni tofauti na OPRAS kwa kuwa unatoa fursa na mawanda mapana kwa mwajiriwa kuweka malengo na shabaha zinazopimika tofauti na mfumo wa OPRAS.

“Kwenye mfumo wa PEPMIS hata sehemu ya majukumu mengine utakayopangiwa na viongozi unaweza kuyaweka na yakapimika”, alisema Kauzen.

Alisisitiza wakuu wa vitivo, wakurugenzi, wakuu wa iadara na viongozi wengine kuwakumbusha wanaowasimamia kujisajikli na kujaza taarifa zao ili wasikose mshahara Mwezi February.

Posted in

Leave a comment