Na Vincent Mpepo, OUT-Songea

Wakristo wametakiwa kuacha wivu kwa kuwa una matokeo mabaya yanayoweza kuleta atahari hasi na uharibufu katika jamii hivyo kutenda dhambi.

Wito huo umetolewa na Padre Guntram Hongo wakati wa mahubiri siku ya Jumamosi katika Kanisa Katoliki, Kigango cha Nambehe Parokia ya Msalaba Mkuu Jimbo Kuu la Songea wakati wa ibada ya kumwombea Marehemu Thobias Komba.

Alisema wivu mbaya hurudisha nyuma maendeleo ya jamii kwa mtu mmoja mmoja, hufarakanisha na ni dhambi.

“Wivu mbaya huleta matokeo mabaya na athahari zake daima ni hasi”, alisema Padre Hongo.

Alisema wivu ni dhambi ambayo inaweza kutendwa na mtu yeyote awe Askofu, Padre, Mtawa au muumini na hivyo kuwataka wakristo kuishi maisha yenye kumpendeza Mungu.

Kwa upande wake, Wilhem Komba alisema wivu una tabia ya kuwafanya watu kuchukia mafanikio ya wengine au kufurahia kushindwa kwa wengine kitu ambacho wakati mwingine ni kikwazo cha maendeleo siyo tu kwa mwenye mafanikio hata mwenye wivu.

“Wivu ni kuzuizi cha maendeleo na mafaniko ya mwenye wivu na wengine”, alisema Komba.

Alisema baadhi ya athari za wivu ni pamoja na mtu kushindwa kujifunza mambo mema kwa waliofanikiwa badala yake kuishia kufurahia anguko au kushindwa kwa wengine kitu ambacho hakina faida chanya.

Msemaji wa Familia Jordan Komba aliwashukuru ndugu, jamaa na marafiki walioshiriki katika ibada ya kumwombea Marehemu na kwamba wamekuwa faraja wakati wote tangu wakati wa homa mpaka alipopatwa na umauti.

Matukio katika picha: Baadhi ya ndugu, jamaa na marafiki wlioshiriki katika ibada ya kumuombea Marehemu Thobias Komba siku ya Jumamosi katika Kanisa Katoliki, Kigango cha Nambehe, Parokia ya Msalaba Mkuu, Jimbo Kuu la Songea(Picha na Vincent Mpepo).

Posted in

Leave a comment