Na Vincent Mpepo, OUT

Jamii imetakiwa kuasili watoto wanaoishi na kutunzwa kwenye vituo mbalimbali ili wawe sehemu ya familia hivyo kupata malezi na uangalizi unaostahili kama wanajamii wengine.

Wito huo umtolewa na Afisa Ustawi wa Jamii, Malezi na Familia wa Jiji la Arusha, Nivoneia Kikaho wakati wa uzinduzi wa chama cha waandishi wa habari wanawake mkoa wa Arusha ‘ARUSHA WOMEN IN MEDIA’ uliofanyika mwishoni mwa wiki na kuhudhuliwa na wanawake waandishi wa mkoa huo, wanafunzi wanawake wa tasnia hiyo na wadao mbalimbali wa maendeleo.

Alisema baadhi ya vigezo vinavyotumika ili anayekusudia kuasili mtoto kupata kibali cha mtoto wa kulea ni pamoja na utayari, maadili, usafi na mapenzi kwa watoto na kuwa utaratibu huo ni wakisheria na una taratibu za kufuata.

“Wanadoa wanakaribishwa kuasili watoto kwa kuwa kuna mazingira rafiki tofauti na wasio kwenye ndoa”, alisema Kikaho.

Alisema uwezo na vigezo vivyokusudiwa ni vya msingi na vya kawaida ambavyo vitamuwezesha mtoto anayeasiliwa kupata mahitaji yake muhimu.

Hatahivyo, alisema bado kuna mwamko mdogo wa jamii kuasili watoto jambo ambalo linahitaji uhamasishaji.

Mwenyekiti Arusha Women in Media Jamillah Omar kuasili mtoto ni kama sadaka hivyo anayeasili hapaswi kuchagua mtoto kati wengi kwenye mahali wanapoishi ili kuzuia unyanyapaa na kuwafanya wanakosa kuasiliwa kujisikia vibaya.

Hatahivyo, kwa uzoefu wa miaka ya hivi karibuni suala la kuasili watoto halijapata kipaumbele na jamii bado kunahitajika juhudi za makusudi kuhamasisha jamii ili ione umuhimu wa jambo hilo.

Posted in

Leave a comment