Na Ruth Kyelula, Mbulu DC

Viongozi wa serikali za mitaa ikiwemo watendaji na wenyeviti wa vijiji, kata na mitaa wametakiwa kutoa ushirikiano kwa shirika la UCRT linalotekeleza mradi wa mpango wa matumizi bora ya ardhi vijinini.

Hayo yalisemwa na Katibu Tawala wa Wilaya ya Mbulu, Paulo Bura kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Mbulu Veronica Kessy wakati akifungua kikao cha uzinduzi wa awamu ya pili ya mradi wa mpango wa matumizi bora ya ardhi kwa vijiji sita chini ya Ujamaa Community Resource Team (UCRT), uliofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya wilaya ya Mbulu Machi 19, 2024.

Alisema viongozi hao wanatakiwa kutoa ushirikiano watekelezaji wa mradi huo ili kile walichokuja nacho kiweze kuwanufaisha wananchi wa wilaya hiyo na kutimiza malengo hayo yenye nia njema.

“Lakini sisi tulioingia kwenye awamu hii vijiji hivi sita, pia tujue sisi ni wa mfano na tunatakiwa tufanye vizuri ili kuwapa moyo wafadhili kuendelea na mradi huu kwa vijiji vingine”, alisema Bura.

Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Hamashauri ya Wilaya ya Mbulu, Petro Tarimo aliwaomba wanufaika wa mradi wa zamani na  wapya waendelee kutoa ushirikiano kwa UCRT na kutoa elimu kwa wanchi wengine ili kuepuka migogoro ya mipaka.

 Mratibu wa Ujamaa Community Resource Team (UCRT), Dismas Meitaya ameushukuru uongozi wa Wilaya Mbulu kwa ujumla kwa ushirikiano wanaoutoa kwa takribani miaka 20 hivyo kuwawezesha kutekeleza mradi huo kwa ufaninsi.

Malengo ya UCRT ni kuwezesha jamii ya asili kumiliki, kusimamia na kunufaika na ardhi, alisema Meitaya

Alisema wamelenga aidi kwenye jamii ya wakusanya matunda, ambao ni wa hadzabe na waakie, wamaasai, wadatoga pamoja na wafugaji , wakulima wabatemi  na wa iraqw.

“Huu mpango ni shirikishi sana, akina mama wanapewa kipaumbele ili washiriki kikamilifu na zaidi kuona jamii na akina mama kupitia vikundi vyao wakiwa mstari wa mbele.

Alibainisha vijiji lengwa sita vya mradi katika bonde la Yaeda na Ziwa Eyasi ni Garbabi, Yaedakati, Dirim, Endalat, Murkuchida na Endamilay.

Posted in

Leave a comment