Na Slyvester Richard, Singida
Mahakama ya Wilaya Singida imemuhukumu Baraka Joel ambaye pia anajulikana kwa jina la Yohana (23), mkulima na mkazi wa Mughamo Manispaa ya Singida kwenda jela miaka 30 kwa kosa la kubaka.
Mshitakiwa Baraka alitenda kosa hilo Februari 17, 2023 huko Mtaa na Kata ya Mughamo, Tarafa ya Ilongero, Wilaya na Mkoa wa Singida ambapo alimbaka mwanafunzi wa darasa la 7 mwenye umri wa miaka 14.
Baada ya kutenda kosa hilo, Mshitakiwa alikamatwa na Jeshi la Polisi na kufikishwa mahakamani Machi 8, 2023 na kesi kusikilizwa na pande zote mbili.
Kutokana na ushahidi uliowasilishwa na upande wa mlalamikaji, ulithibitisha mshitakiwa alitenda kosa hilo hivyo Mahakama kutoa adhabu hiyo Machi 14, 2024 mbele ya Mh. Hakimu Robert Uguda.
Posted in Uncategorized
Leave a comment