Kaimu Mkuu wa Dawati la jinsia na watoto Wilaya ya Singida Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Exaud Waya akitoa elimu juu ya ukatili wa kijinsia kwenye kongamano la watoto waishio katika mazingira magumu katika ukumbi wa Vatican maeneo ya Mwenge, Manispaa ya Singida.

Na Sylvester Richard -Singida

Kaimu Mkuu wa Dawati la jinsia na watoto Wilaya ya Singida Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Exaud Waya amesema kuwa ndoa na mimba za utotoni ni chanzo  cha watoto waishio katika mazingira magumu.

Amesema hayo Aprili 17, alipokuwa anatoa elimu juu ya madhara ya ukatili wa kijinsia kwa jamii kwenye kongamano la kimataifa siku ya watoto wa mitaani lilofanyika kwa ngazi ya Wilaya kwenye ukumbi wa Vatican, uliopo Mtaa wa Mwenge , Manispaa ya Singida.

Alimesema yapo mambo mengine yanayochangia ongezeko la watoto waishio katika mazingira magumu ikiwemo wazazi kushindwa kutoa huduma muhimu kwa watoto wao, watoto kufanyiwa ukatili majumbani kwao, wazazi kugombana, wazazi wa kiume kukataa mimba au watoto, utumiaji wa dawa za kulevya kiholela na magonjwa kama vile VVU/UKIMWI.

Aidha amewasihi wazazi kulea familia zao katika maadili na kuwasisitiza kumcha Mungu kila mmoja kulingana na imani yake jambo ambalo litasaidia kujenga taifa imara lisilokwa na watoto waishio katika mazingira magumu.

Naye Sajenti wa Polisi Abihudi Kasonde kutoka kikosi cha usalama barabarani Singida ambaye pia amehudhuria kongamano hilo, amewaelimisha washiriki juu ya usalama barabarani ikiwemo mbinu za kuepuka ajali wakati wa kutumia barabara .

Pichani ni watoto wakishiriki wa kongamano la watoto waishio katika mazingira magumu katika ukumbi wa Vatican uliopo Mtaa wa Mwenge Manispaa ya Singida.

Posted in

Leave a comment