Na Mwandishi wetu, Dar es salaam
Kanisa la DPA la jijini Dar es salaam litafanya maadhimisho ya miaka minne tangu kuanzishwa kwake kama sehemu tathimini na shukrani kwa Mungu.
Hayo yamebainishwa na Mchungaji muasisi wa kanisa hilo, Hanington Kabuta wakati wa mahojiano na mwandishi wetu huku akitanabaisha kuwa madhabahu hiyo ya DPA imekuwa baraka kwa mtu mojamoja na jamii kwa ujumla na kwamba Mungu amewatendea mengi.
“Mwezi huu wa nne mwaka 2024 kanisa letu la DPA limefikisha miaka 4 tangu lianzishwe hapa Goba, Tegeta A, Mtaa wa Msabila”, alisema Mchungaji Kabuta.
Alisema uongozi wa kanisa hilo umeamua kufanya maadhimisho ndani ya wiki hii, ambapo kilele chake ni Jumapili jioni.
Tuna maombi ya mfungo wiki hii pamoja na Semina ya Historia ya Kanisa Kiulimwengu, Afrika, Tanzania, na Hatimaye DPA, alibanisha Mchungaji Kabuta.
Aliongeza kuwa semina ni Jumatano tarehe 24 hadi Junapili tarehe 28/04/2024 na Muda ni kuanzia saa 10:00 Jioni hadi 12:30 Jioni kwa siku hizo tano huku agenda kuu ni ‘Fundisho la Kanisa, Maombi na Maombezi.
Aliwataka watu wote wenye mapenzi mema kuhudhuria na kuwaalika wengine huku akiwakumbusha kushirikisha taarifa hii kwenye mitandao ya kijamii ili wengi waokolewe.

Leave a comment