RC Dendegu Kuimarisha Ushirikiano na TCCIA

Na Sylvester Richard, Singida

Mkuu wa Mkoa wa Singida Halima Dendegu akiongea na wajumbe kutoka Chama cha Wafanyabiashara, Wakulima na wenye Viwanda Tanzania (TCCIA) Mkoa wa Singida kwenye kikao kilichofanyika ofisini kwake leo.

Mkuu wa Mkoa wa Singida Halima Dendegu ameuhakikishia uongozi wa Jumuiya ya wafanyabiashara (TCCIA) Mkoa wa Singida kuimarisha ushirikiano kati ya Serikali na sekta binafsi ikiwemo wafanyabiashara   ili kuinua uchumi wa Mkoa wa Singida kwakuwa Serikali ya Mkoa ipo imara katika suala zima la ulinzi na usalama.

Dendegu alitoa kauli hiyo Aprili 24, 2024 ofisini kwake wakati wa mazungumzo na kati yake na uongozi wa chama cha wafanyabiashara, wakulima na wamiliki wa viwanda Tanzania (TCCIA) waliopo Mkoani Singida.

Alisema Jumuiya hiyo ni muhimu na muhimili katika kuinua uchumi wa Singida hivyo kuwaomba kuendeleza ushirikiano huo kwa ajili ya maendeleo ya wananchi wa mkoa huo.

 ambao Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassani amedhamiria kuboresha maisha ya mtu mmoja mmoja na ndiyo maana miradi mbalimbali inatekelezwa.

Akiongea kwa niaba ya TCCIA, Mwenyekiti wa Chama hicho Bw. Elly Kitila Mkumbo alisema walifika  ofisini hapo kwa lengo la kukitambulisha chama hicho cha wafanyabiashara kwa Mkuu wa Mkoa aliyehamia hivi karibuni akitokea Mkoa wa Iringa ambapo wajumbe walipata nafasi ya kujadili masuala  mbalimbali kuhusu kukuza uchumi kupitia  sekta binafsi ikiwemo biashara.

Alisema chama hicho kitaendeleza na kudumisha ushirikiano kati yake na serikali kwa madhumuni ya kumkomboa na kumhakikishia mfanyabiashara mazingira wezeshi katika shughuli zake kwa maslahi ya taifa pamoja na kulitangazo soko la kimataifa la vitunguu lililopo Mkoani Singida.

Mwenyekiti wa Wafanyabiashara, Wakulima na wenye Viwanda Tanzania (TCCIA) Mkoa wa Singida Bw. Elly Kitila Mkumbo, akizungumza kwenye kikao baina ya Mkuu wa Mkoa wa Singida na TCCIA kilichofanyika ofisini kwa Mkuu wa Mkoa huo.

Posted in

Leave a comment