
Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe. Halima Dendego akiongea na watumishi wa umma Mkoa wa Singida katika kituo cha mabasi Ikungi kwenye maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani.
Na Sylvester Richard-Singida
Mkuu wa Mkoa wa Singida Halima Dendego amewataka watumishi wa umma Mkoa wa Singida kuisikiliza na kuielewa hotuba Mh.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassani iliyowasilishwa kwa niaba yake na Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango kwenye maadhimisho ya Mei Mosi 2024 yaliyofanyika kitaifa Mkoani Arusha.
Dendego amebainisha hayo jana Mei 1, 2024 wakati akizungumza na watumishi wa umma kwenye maadhimisho ya siku ya wafanyakazi Duniani yaliyofanyika kimkoa kwenye kituo cha mabasi Wilayani Ikungi.
Baadhi ya mambo yaliyoahidiwa na serikali kwa wafanyakazi kupitia hotuba hiyo ni pamoja na kuhuisha viwango vya mishahara kwa kuzingatia uwezo wa kiuchumi na kibajeti pamoja na ujuzi na utendaji wa waajiriwa misingi ambayo imetajwa kuwa ni muhimu ili kuepuka mfumuko wa bei na uhimilivu wa deni la taifa na athari nyiningine za kichumi.
Aidha, Dendego amewakumbusha watumishi kufanya kazi kwa kuzingatia kanuni na maadili ya kazi ili kuongeza ufanisi katika kazi. Maadhimisho hayo yalibebwa na kaulimbiu isemayo “Nyongeza ya mshahara ni msingi wa mafao bora na kinga dhidi ya hali ngumu ya maisha” na yaliambatana na utoaji wa zawadi ambapo Dendegu alikabidhi zawadi mbalimba kwa wafanyakazi wa Mkoa wa Singida waliofanya vizuri mwaka 2024.
Leave a comment