Na Vincent Mpepo, Kwembe

Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) kampasi ya Mloganzila kimewataka Wananchi wa Kwembe na maeneo jirani kuchangamkia fursa ya kambi maalumu ya kupima afya bure ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa Elimu ya Juu kwa mageuzi ya kichumi (HEET).

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kwembe Rajabu Koba wakati wa mkutano wa wa kwanza na wa wananchi wa Mtaa huo uliofanyika jana katika ofisi za mtaa huo ambapo masuala mbalimbali yalijadiliwa ikiwemo suala la kambi hiyo maalumu itakayofanyika Tarehe 26-27 Februari 2025 kuanzia Saa 03:00 asubhi mpaka saa 10:00 alasiri.

Koba alisema chuo hicho kimewajulisha kuhusu kambi hiyo na kuwataka wananchi kuitumia fursa hiyo ili kufanya uchunguzi wa afya zao.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo imetaja huduma kadhaa zitakazolewa ikiwemo uchunguzi wa awali wa magonjwa ya macho, masikio, pua na koo.

“Huduma nyingine ni pamoja na uchunguzi wa kinywa na meno, saratani ya matiti na shingo ya kizazi, homa ya ini na tezi dume kwa kipimo cha damu”, imenukuliwa taarifa hiyo.

Aidha taarifa hiyo imeongeza kuwa kutakuwa na elimu kwa umma kuhusu madhara yanayotokana na matumizi ya dawa na usugu wa dawa, magonjwa ya kuambukizwa, lishe na uchakataji wa taarifa kwa kutumia akili mnemba.

“Wananchi watapata fursa ya kujionea bidhaa mbalimbali zinazotengenezwa na wataalamu kutoka famasia na tiba asilia”, ilisema taarifa hiyo.

Wakati huohuo, Koba aliwataka wananchi wa Mtaa huo kuchangamkia fursa za ujasiriamali katika mradi mkubwa unaotarajiwa kuanza hivi karibuni katika eneo la Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) kampasi ya Mloganzila.

“Wanacnhi wa maeneo jirani wajiandae kwa kazi mbalimbali ikiwemo vibarua na ujasiriamali kama mama lishe katika mradi huo”, alisema Koba.

Alisema fursa hizo ni matokeo ya utekelezaji wa Mradi wa Elimu ya juu kwa Mageuzi ya Kichumi unaofadhiliwa na Benki ya Dunia unahusisha ujenzi wa majengo sita ambapo tayari kandarasi zimekwishatolewa kwa makampuni mawili na utagharimu kiasi cha Dola za Kimarekani milioni 30.5.

Posted in

Leave a comment