Na Vincent Mpepo, OUT

Imeelezwa kuwa utekelezaji wa malipo ya mafao sanjali na kikokotoo kwa wastaafu ni matokeo ya tafiti mbalimbali ambazo zilionesha ya ulipaji kidogokidogo badala ya kulipa kwa mkupuo unaweza kusaidia zaidi wastaafu tofauti na ilivyokuwa hapo awali.

Hayo yamebainishwa na Katibu Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Elimu ya Juu Taifa, Elia Kasalile wakati wa Mkutano Mkuu wa Tawi la chama hicho la Chuo Kikuu Huria cha Tanzania uliofanyika leo katika ukumbi wa chuo hicho jijini Dar es salaam.

Alisema matokeo ya tafiti na mapendekezo yalionesha kuwa sehemu kubwa ya wastaafu hawakuwa na uwezo wa kuzitawala pesa zao walizolipwa kwa mkupuo badala yake wengi wao haikuzidi miaka mitatu walimaliza na kuzalisha matatizo mengine ikiwemo kifo.

Alianisha changamoto nyingine zinazowakabili wastaafu ikiwa ni pamoja na kupungua kwa kiasi cha kipato na idadi ya marafiki hivyo kuwabadilishia mfumo wa mfumo wa maisha ambapo mstaafu asipojiandaa inakuwa janga.

“Nawakumbusha wanachama kuunga mkono juhudi za chama chetu kupitia programu mbalimbali ikiwemo upatikanaji wa viwanja vya ujenzi kama njia mojawapo ya dhidi ya majanga ikiwemo kutegemea malipo ya kustaafu kustaafu kujenga”, alisema Kasalile.

Alisema matokeo ya tafiti yalizingatia vigezo vya kitaifa na kimataifa kupitia shirika la kazi (ILO) yalipendekeza kiwango cha mafao kwa mkupuo kipunguzwe na badala yake pesa hiyo ilipwe kwenye nyongeza ya kila Mwezi.

Aidha aliukumbusha uongozi wa chama hicho chuoni hapo kuingia makubaliano na menejimenti ili kupata ada ya uwakala kupitia wafanyakazi wasio wanachama wa chama hicho kwa kuwa ni wanufaika wa juhudu za kulinda na kutetea maslahi mbalimbali.

Mwenyekiti wa Chama hicho chuoni hapo, Salatiel Chaula alisema chama chake kimeendelea kulinda na kutetea maslahi ya wanachama wake licha ya changamoto mbalimbali ikiwemo uhaba wa fedha katika uendeshaji wa chama hicho.

Kwa upande mwingine, aliushukuru uongozi wa chuo hicho kwa ushirikiano ambao umesaidia katika ufumbuzi wa changamoto mbalimbali za kulinda na kutetea a ya wafanyakazi.  

Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Rasilimali watu chuoni hapo, Bi Joyce Kimati aliwakumbusha wafanyakazi kufuata sheria, taratibu na kanuni za kazi ikiwemo kujaza taarifa za kazi na majukumu yao katika mfumo wa Usimamizi na Utendaji kazi katika utumishi wa Umma (PEPMIS) kwani kutokufanya hivyo ni kujiletea matatizo.

Posted in

Leave a comment