
Na Cartace Ngajiro, Tanga
Menejimenti ya Bandari ya Tanga imewahakikishia wadau wa bandari hiyo kuendelea kutoa ushirikiano katika masuala mbalimbali ya kibandari ikiwa ni pamoja na utoaji huduma bora kwa wateja ili kuongeza tija na ufanisi.
Kauli hiyo imetolewa na Kaimu Meneja wa Bandari ya Tanga Bw. Peter Millanzi hivi karibuni wakati akifunga kikao cha maboresho ya Bandari ya Tanga ‘Tanga Port Improvement Committee’ kilichofanyika jijini Tanga katika ukumbi wa mikutano ulipo katika jengo la Bandari House.
“Ushirikiano uliopo uendelee kuwepo kwani ndio chachu ya mafanikio katika bandari hiyo kiufanisi”, alisema Millanzi.
Aidha aliwaahidi wadau hao kufanyia kazi na kupatikana kwa ufumbuzi kwa changamoto zilizopo ili kuendelea kuvutia wateja zaidi kutumia bandari hiyo.

Leave a comment