Na Vincent Mpepo

Wakati dunia ikiadhimisha Siku ya Wafanyakazi duniani (Mei Mosi), wafanyakazi wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania wameungana na wenzao duniani kuelezea matarajio yao kwa serikali na uongozi wa chuo huku wakitegemea maboresho kwenye mazingira bora ya kazi.

Akizungumza na Mwandishi wetu, Mhadhiri Msaidizi katika Idara ya Habari na Masomo ya Ukutubi chuoni hapo, Azizi Kagugu alisema anatarajia kuwepo kwa mazingira bora na wezeshi yatakayosaidia ufanyaji kazi kwa tija kwa mendeleo ya taasisi, familia na jamii kwa ujumla.

Mjumbe wa Halmashauri Mkutano Mkuu Taifa, Ntimi Kasumo, aliwapongeza wafanyakazi wote waliofika Biafra-Kinondoni jijini Dar es salaam ili kuungana na wengine kwenye maandano yatakayofanyika katika Viwanja vya Tanganyika Packers-Kawe.

Mwenyekiti wa Chama cha Wafanayakazi wa Taasisi za Elimu ya Juu (THTU) Tawi la Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, Salatiel Chaula alisema kwa kuwa Mwaka 2025 ni mwaka wa uchaguzi wanatarajia kupata viongozi watakaokumbuka masuala mbalimbali ya wafanyakazi hususani uboreshaji wa maslahi ikiwemo mishahara.

“Wafanyakazi ni miongoni mwa wapiga kura, tunatarajia uboreshaji wa maslahi na stahiki nyingine”, alisema Chaula.

Akizungumza kwa niaba ya menejimenti ya chuo, Afisa Rasilimaliwatu, Bi Joyce Kimati alisema chuo kinatambua na kinathamini mchango wa wafanyakazi katika kuendeleza shughuli mbalimbali za taasisi hiyo na aliwakumbusha kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za utumishi wa umma.

“Mimi kama mwanachama mwezenu niwapoze ambao mmefanikiwa kuja kushiriki hapa kwa ajili ya maadhimisho haya”, alisema Bi. Kimati.

Maadhimisho ya Mei Mosi kitaifa yatafanyika mkoani Singida yakiwa na kaulimbiu isemayo ‘Uchanguzi Mkuu 2025: Utuletee viongozi wanaojali haki na maslahi ya wafanyakazi wote, sote tushiriki’.

Wafanayakazi wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania wa Mkoa wa Pwani na Dar es salaam katika picha ya pamoja Leo katika Makao Makuu ya chuo hicho kabla ya kuelekea Viwanja vya Tanganyika Packers-Kawe ambako maadhimisho hayo yatafanyika kimkoa.

Wafanyakazi wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania kituo cha Mkoa cha chuo hicho Mkoani Simiyu wakionesha furaha yao Siku ya Mei Mosi: Afisa Tehama, Erasmus Rukantabula, Afisa Tehama na Afisa Udahili, Judith Erasto katika picha ya pamoja.

Posted in

Leave a comment