Serikali imesema kupatikana kwa vifaa vya utafiti wa maji chini ya ardhi kuongeze tija katika masuala ya tafiti ili maeneo yenye changamoto ya upatikanaji wa maji yapate huduma hiyo muhimu.

Kauli hiyo ilitolewa jana na Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) kwa wataalamu wa Mabonde na wakati wa kukabidhi vifaa vya kisasa vya utafiti vilivyonunuliwa kwa fedha ya UVICO na kuwataka wafanye tafiti ili kupata majibu na suluhu endelevu ya upatikanaji wa huduma ya maji kwa wananchi.

“Vifaa hivi viwe chachu ya kuwaongezea uwezo wataalamu wetu na kuweka nguvu katika utafiti ili maeneo yaliyokuwa na changamoto ya upatikanaji wa maji yapate  maji”, alisema Waziri Aweso

Mkurugenzi wa Idara ya Rasilimali za  Maji  Dkt. George Lugomela amesema vifaa hivyo vitawezesha kuchunguza uwepo wa miamba inayohifadhi maji kwa ufanisi hadi kina cha urefu wa mita 1000.

Vifaa hivyo ni pamoja na kifaa cha kuchunguza mipasuko katika miamba kwa njia ya sumaku (Magnetrometer), kifaa cha kuchunguza maji (terrameter), kifaa cha kupima kina cha maji (deeper), kifaa cha kuchunguza mikondo ya maji na kifaa cha kuchukua majira (GPS).

Dkt. Lugomela amemshukuru Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuwezesha kwa fedha zitakazosaidia  kutimia kwa azma ya upatikanaji wa huduma ya maji kwa wananchi kwa asilimia 85 vijijini na 95 mjini ifikapo 2025.

Mgawanyo wa vifaa hivyo uliyagusa mabonde tisa ya maji nchini

Posted in

2 responses to “Vifaa vya Utafiti wa Maji chini ya Ardhi Nchini Vyaongezwa”

  1. Sylvester Machibya avatar
    Sylvester Machibya

    Asante kwa kuendelea kutuhabarisha na kutuelimisha. Kazi inaonekana.

    Like

    1. mpepovincent0 avatar
      mpepovincent0

      Asante kwa kuendelea kuwa msomaji wa ukurasa huu

      Like

Leave a comment