Na Gloria Maganza, Dodoma

Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Damas Ndumbaro amesema katika Kipindi cha miaka minne ya serikali   imefanikiwa kupunguza mrundikano wa wafungwa na mahabusu kwenye magereza hapa nchini ambapo amesema magereza hapa nchini zina uwezo wa kuchukua wafungwa na mahabusu 28,000 nchi nzima.

Waziri Dkt. Ndumbaro ametoa taarifa hiyo leo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio ya Wizara yake katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wa serikali ya awamu ya sita Jijini Dodoma.

Alisema kupitia Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia (MSLAC) jumla ya halmashauri 180, kata 1,907 na vijiji/mitaa 5,702 zilifikiwa na jumla ya wananchi milioni 2,698,908 walifikiwa na kupata elimu na huduma za kisheria kupitia mikutano ya ana kwa ana.

 Lalisema Wizara kupitia Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali imekamilisha uhakiki wa mwisho wa Sheria Kuu 300 kati ya 446 zilizotafsiriwa kwa lugha ya Kiswahili.

“Hii ni sehemu ya jitahada za serikali katika kuimarisha utawala bora, utawala wa sheria na kuimarisha misingi ya utoaji haki” alisema Dkt. Ndumbaro.

Alisema mashauri yenye umri mrefu mahakamani ni 2,780 sawa na asilimia 4 ya mashauri yote yaliyobaki mahakamani hivyo, Tanzania ni miongoni mwa nchi chache barani Afrika zenye mrundikano mdogo wa mashauri mahakamani.

Sanjari na hayo, Waziri Dkt. Ndumbaro amesema mahakama inafanya utaratibu wa  kutumia mfumo wa kutafsiri katika mahakama zote zenye miundombinu ya mtandao (intaneti) nchini ili kuhakikisha haki inapatikana kwa wakati na gharama nafuu.

Posted in

Leave a comment