
Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko, akizungumza na wadau wa kemikali bashirifu zaidi ya 40 wakati akifungua kikao cha wadau wa Kemikali Bashirifu na Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kilichofanyika katika hoteli ya Golden Tulip, Dar es Salaam, Mei 28, 2025.
Na Okello Thomas
Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali imewakumbusha wadau wanaojihusisha na shughuli za kemikali kuhakikisha wanazingatia matumizi salama ya kemikali na kutojihusisha na uchepushwaji wa kemikali bashirifu kwa ajili ya utengenezaji wa dawa za kulevya.
Akizungumza wakati akifungua kikao kilichofanyika katika Hotelk ya Golden Tulip jijin Dar es salaam, Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko amewataka wadau wa kemikali kushirikiana na Mamlaka za Udhibiti ili kutokomeza uchepushwaji wa kemikali bashirifu kwa ajili ya matengenezo ya dawa za kelevya kwani dawa za kulevya huleta athari za kiuchumi, nguvu kazi na kuporomoka kwa maadili.
“Nia ya Serikali ni kuhakikisha kuwa inatokomeza uingiaji, utengenezaji na matumizi ya dawa za kulevya nchini”, alisema Dkt. Mafumiko.
Alisema ili malengo hayo yatimie ni lazima kuziba mianya yote inayochangia masuala hayo kufanyika kila mmoja wetu katika jamii awajibike.

Mkurugenzi wa Huduma za Udhibiti kutoka Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Daniel Ndiyo, akiwasilisha mada kuhusu udhibiti wa kemikali bashirifu kwa wadau wa hao wakati wa kikao kilichofanyika katika hoteli ya Golden Tulip, Dar es Salaam, Mei 28, 2025.
Kamishna wa Ukaguzi na Sayansi Jinai kutoka Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya, Domician Mutayoba alisema kupitia Mamlaka za Udhibiti wanahakikisha wanatengeneza ushirikiano imara na wadau ili kuzuia na kudhibiti uchepushwaji wa kemikali bashirifu zisitumike katika utengenezaji wa dawa za kulevya na silaa.
Kwa upande wake Meneja wa Total Med-Lab Solutions, Shaphii Miraji ameishauri Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kuendelea kutoa elimu kwa wadau wa kemikali kwani teknolojia inabadilika hivyo elimu endelee kutolewa ili kuboresha masuala ya kemikali nchini.

Wadau wa Kemikali bashirifu kutoka kampuni mbalimbali wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zinawasilishwa katika kikao baina ya Mamlaka na wadau hao kilichofanyika katika hoteli ya Golden Tulip, Dar es Salaam, Mei 28, 2025.

Leave a comment