Madereva wa Serikali Wakumbshwa Nidhamu Barabarani

Na Issa Mwandagala, Songwe

Madereva wa magari ya serikali pamoja na taasisi za umma Mkoani Songwe wamekumbushwa kuwa na nidhamu na kuzingatia sheria za usalama barabarani ikiwa ni pamoja na kuwashauri wa viongozi wanaowaendesha ili kupunguza ajali zinazoweza kuepukika ikiwa pamoja na kulinda usalama wa watumiaji wengine wa barabara.

Rai hiyo imetolewa Mwanzoni mwa Mwezi Juni na Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Songwe Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP), Charles Bukombe wakati wa semina ya utoaji wa elimu ya usalama barabarani kwa madereva hao katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Songwe.

SSP Bukombe alifafanua wajibu wa dereva ambao ni kufuata sheria, alama na michoro ya barabarani ili kuwa salama katika majukumu yao ya kila siku.

Aliwaasa madereva hao kujiendeleza kitaaluma kutokana na kutokana na mabadiliko ya teknolojia ambayo inawataka kujipanga wakati na baada ya maisha ya kazi kwa mstakabali wa maisha yao baada ya kazi.

Kwa upande wake, Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Wilaya ya Mbozi, Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Anton Sabasaba alisema malengo ya semina hiyo ni kuwaelimisha madereva juu ya athari za mwendokasi, kuvipita vyombo vingine sehemu ambazo haziruhusiwi na kuchukuwa tahadhari katika makazi ya watu ili kuepusha ajali.

Vilevile katika semina hiyo, madereva hao walipata wasaa wa kukumbushwa sheria mbalimbali za usalama barabarani na

Koplo Chika Sanda na Koplo Maganga Kalulumya kutoka Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Songwe waliwakumbusha madereva sharia mbalimbali za usalama barabarani na kuwataka kuwa na kitabu cha sheria hizo ili kujikumbusha na kuwa salama kipindi chote cha utendaji wa majukumu yao ya kila siku.

Akizungumza kwa niaba ya madereva, Fungafunga Njovu ambaye ni dereva kutoka Halmashauri ya Mji wa Tunduma alilishukuru Jeshi la Polisi Mkoa wa Songwe kwa elimu waliyoipata na ameomba mafunzo hayo yawe endelevu ili kuendelea kuwajengea uelewa juu ya umuhimu wa sheria za usalama barabarani.

Posted in

Leave a comment