Kwaya ya watoto wa shule ya Jumapili wakihudumu katika ibada SiKu ya Jumapili (picha na Vincent Mpepo).

Na Vincent Mpepo

Mtenda Kazi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Anna Mauki amewataka washarika wa kanisa hilo kuona fahari ya umoja wa makanisa yaliyoungana na kuwa kanisa moja kwa kuwa ndani yake kuna mafanikio mengi.

Bi. Anna Mauki aliyasema hayo Siku ya Jumapili wakati wa mahubiri na kuwataka wakristo wa sasa kuona kuwa wana sehemu ya kufanya ili kuhakikisha historia ya kanisa hilo kwa miaka 62 ijayo inakuwa na kumbukumbu nzuri zaidi kwa wao kuhusika katika mambo mbalimbali.

Alisema waasisi wa umoja huo walifanya vitu na maono yao ndiyo yanayoonesha mafanikio ya kanisa kwa sasa kupitia kazi, shughuli na huduma mbalimbali zilizopo akitaja baadhi kama hospitali, vyombo vya habari, shule za msingi na sekondari pamoja na vyuo vikuu ambavyo vinamilikiwa na kanisa na vina mchango kwa jamii.

“Tupende kazi za umoja kwakuwa ni kazi za Mungu”, alkisema Bi.Mauki.

Alisema kanisa liendelee kuwaandaa watoto kuja kuwa wakristo wawajibikaji siku zijazo na kwamba maanadalizi hayo huanzia katika ngazi ya familia.

“Kanisa lina utaratibu mzuri wa kuwapokea watoto tangu wakiwa wadogo na limeendelea na programu mbalimbali katika makuzi yao mpaka utu uzima”, alisema Bi.Mauki.

 Alisema na bado familia ina wajibu mkubwa kuhakikisha inafuatilia makuzi na mwenendo wa mtoto ili awe mkristu mwajibikaji.

Aidha aliwataka wakristo kuacha tabia ya kufuatilia mambo yasiyowahusu na badala yake wajikite katika yanayowahusu.

Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi Mtaani hapo, Exaud Mchome alitoa taarifa ya maendelep ya ujenzi na kwamba kwa kwa wiki ile ujenzi haukuenda vizuri kutokana na mafundi wanaofanya kazi hiyo kutofikia viwango stahiki.

Aliwashukuru washarika kwa kuendelea kujitoa kwa ajili ya kazi ya ujenzi unaoendelea kanisani hapo na kusisitiza ambao bado hawajakamilisha ahadi zao kwa awamu ya kwanza ya Januari hadi Juni kukamilisha ili kupisha zoezi la mavuno lililopo mbele.

Wakati huo huo, Mwinjilsti Kiongozi wa Mtaa huo, Emeline Mnzava aliwashukuru wazazi waliowaruhusu vijana wao kushiriki Tamasha la Twenzetu kwa Yesu kwani licha ya kuwa ni mtoko ni sehemu ambayo imewapa mafunzo yatakayowasaidia kuikulia Imani.

Aidha, aliwakumbusha washarika kuendelea kutoa sadaka ya mfuko wa elimu kwa kuwa ina majukumu ya kusaidia watoto wengi kupata elimu.

Posted in

Leave a comment