Na Tabia Mchakama

Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) imeshuhudia ulipwaji wa fidia kwa Bi. Bahati Ngowi kufuatia kufuatia kifo cha mume wake Profesa Ngowi aliyepata ajali ya gari maeneo ya Mlandizi Kibaha mkoani Pwani tarehe 28 Machi 2022.

Akishuhudia tukio hilo Kamishna wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania, Dkt. Baghayo Saqware alizitaka kampuni za bima kuhakikisha zinalinda na kutetea haki za wateja wao wa bima wanapopatwa na majanga ili kuleta utulivu na ahueni kwa waathirika.

Aidha alimshukuru Mhe. Waziri Mkuu, Kassimu Majaliwa kwa kumuelekeza mhanga huyo mahali sahihi lakini na kuipongeza kampuni ya bima ya Mayfair kwa kumpatia mama huyo fidia stahiki iliyoendana na janga bila ya usumbufu wowote.  

“Ninawaalika watanzania kuja TIRA ikiwa mtakutana na changamoto yoyote ya kibima”, alisema Kamishna Dkt. Saqware.

Kwa upande wake, mnufaika wa bima, Bi. Bahati Ngowi alisema TIRA imekuwa msaada mkubwa kwa sababu alianza kufuatilia madai hayo mahakamani mara baada ya ajali kutokea na mwaka 2025 alielekezwa kufika TIRA na Mhe. Waziri Mkuu wa Tanzania, Majaliwa Kasim Majaliwa.

Kampuni ya bima ya Mayfair imemlipa Bi. Bahati Ngowi kiasi cha shilingi milioni mia moja na arobaini na tano (145,000,000).

Posted in

Leave a comment