
Na Vincent Mpepo
Wanawake walio kwenye ndoa wametakiwa kuwasaidia waume zao katika majukumu ya kifamilia kwa kufanya kazi badala ya kuwa wategemezi na walalamishi ili kuwapunguzia msongo wa mawazo na vifo waume zao.
Kauli hiyo imetolewa jana na Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Kiinjili Kilutheri Tanzania (KKKT), Ismail Mwipile wa Usharika wa Segerea jijini Dar es salaam wakati wa mahubiri ya ibada ya ndoa ambapo Mfanyakazi wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania Stewart Kaberege alifunga pingu za masiha na Bi Suzana Kweka.
Alisema kwa miaka ya hivi karibuni kumekuwa na ongezeko la wajane linatokana na changamoto za ndoa ambazo kwa kiasi fulani zinasababisha na msongo wa mawazo kwa wanaume kutokana na kuzidiwa kimawazo, majukumu na wakati mwingine kutopata msaada kutoka kwa wake zao.
“Niwakumbushe wanawake mlio kwenye ndoa kuwatii, kuwaheshimu na kuwasaidia waume zenu majukumu ili mzeeke pamoja”, alisema Mchungaji Mwipile.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, Profesa Alex Makulilo ambaye aliongoza wafanyakazi wa chuo hicho katika hafla za sherehe ya ndoa ya Stewart Kaberege alisema ndoa si jambo lelemama kwani linahitaji wawili walioamua kuishi pamoja kuwa na akili za ziada.

Aliwapongeza maharusi hao kwa hatua hiyo muhimu na kuwataka kuishi kwa kadiri ya maelekezo ya dini na Imani yao.
Aidha aliwaasa kuzaa watoto wengi ili kuijaza dunia kama maandiko yanavyowataka wakristo kufanya hivyo.
“Stewart na mkeo msijibane sana, nendeni mkazae kuijaza dunia”, alisema Profesa Makulilo
Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi, Ntimi Kasumo aliwakaribisha wageni na kuwashukuru kwa michango yao ya hali na mali ambayo imesaidia kufanikisha hafla hiyo na kwamba alisimia 20 ya michango hiyo imewekwa kwenye akaunti ya maharusi hao kama zawadi.
Uchunguzi uliofanywa na mwandishi umebaini kutokuwepo kwa umoja kati ya wafanyakazi wa chuo hicho husasani kati ya watumishi wanataaluma na waendeshaji kutokuwa na mizania katika matukio mengi ya kijamii.

Leave a comment