
Na Issa Mwadangala.
Madereva wa vyombo vya moto wanaofanya safari zao Barabara ya Mbeya-Tunduma wametakiwa kuacha tabia ya kuendesha vyombo hivyo kwa mazoea ili kupunguza ajali za barabarani.
Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Raphael Magoma aliyasema hayo jana wakati akitoa elimu kwa madereva na abiria katika eneo la ukaguzi wa magari lililopo Chimbuya Wilaya ya Mbozi Mkoa wa Songwe huku akiwataka kufuata sheria na miongozo ya usalama barabarani.

“Mnapaswa kujitathmini na kuacha tabia ya kufanya kazi kwa mazoea”,alisema Magoma.
Alisema kila safari ni ya kipekee na inahitaji umakini wa hali ya juu kulinda maisha maisha ya watu wasio na hatia.
Aidha, aliwataka madereva hao kuzingatia sheria za usalama barabarani ikiwemo kutozidisha mwendo, kutoendesha wakiwa wamelewa na kuhakikisha vyombo vyao vya usafiri vipo katika hali nzuri kabla ya safari.
“Ninawataka abria mtoe taarifa kuhusu madereva wazembe ili hatua za haraka zichukuliwe dhidi yao”, alisema Magoma.

Leave a comment