Na Mwandishi Wetu

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Ally Ussi amempongeza Waziri wa Fedha Dkt. Mwigulu Nchemba kwa usimamizi madhubuti na utoaji wa fedha katika miradi mbalimbali ya maendeleo nchini. 

Ussi alitoa pongezi hizo wakati wa ukaguzi na uwekaji wa jiwe la msingi katika ujenzi wa daraja la Konkilangi na barabara ya maingilio kiwango cha changarawe yenye urefu wa Km 1.5 katika Wilaya ya Iramba Mkoani Singida.

Alisema pongezi hizo ni matokeo ya ustawi wa jamii kiuchumi kutokana na usimamizi mzuri wa fedha za maendeleo zinazotolewa na serikali katika utekelezaji miradi ya maendeleo nchini ambayo imekuwa na matokeo chanya.

“Tumeona hayo katika miradi ya ujenzi wa miundombinu ya katika sekta za maji, afya, elimu, umeme na kadhalika”, alisema Ussi.

Alisema kazi hiyo nzuri inatokana na wajibu anaobeba kumsaidia Rais katikakuhakikisha wanafikiwa na huduma muhimu.

Waziri wa Fedha Dkt. Mwigulu Nchemba alisema serikali imedhamiria kusogeza huduma zote muhimu wa wananchi kwa kuzingatia utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) 2020-2025 na imefanya kwa kiwango kinachostahili.

Alisema Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amekuwa kiongozi imara katika kushughulikia changamoto zinazowakabili Wananchi wote Nchin kwa kuboresha mazingira ya huduma hizo muhimu kwa maendeleo ya Taifa

Mbio za Mwenge wa Uhuru 2025 zimeongozwa na Kauli mbiu isemayo ‘Jitokeze Shiriki Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025 kwa amani na Utulivu’.

Posted in

Leave a comment