Na Issa Mwadangala, Songwe

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Augustino Senga, ameongoza matembezi kwa vyombo vya usalama mkoani humo Julai 25, 2025.

Akizungumza mara baada ya mazoezi hayo ya utimamu wa mwili, Kamanda Senga alisema kuwa lengo la mazoezi hayo ni kujenga umoja, ushirikiano na kuimarisha afya ya mwili na akili kwa vyombo vya ulinzi na usalama Mkoani humo.

Aidha, Kamanda Senga alizungumzia umuhimu wa afya njema kama nguzo muhimu katika utendaji wa kazi na maisha kwa ujumla na kuwahimiza Askari na Watumishi wengine kupenda kufanya mazoezi kwa faida ya afya zao.

“Afya bora ni msingi wa ufanisi kazini na maisha ya baadaye”, alisema Kamanda Senga

Alisema ni mihimu kuhakikisha kuwa mwili na akili imara si tu kwa ajili ya sasa bali pia kwa maisha baada ya kustaafu.

Katika matembezi hayo wadau mbalimbali kutoka vyombo vya ulinzi na usalama walishiriki ikiwemo Jeshi la Wananchi wa Tanzania, Jeshi la Kujenga Taifa, Jeshi la Magereza, Jeshi la Zimamoto na Uokozi pamoja na Ofisi ya Rais.

Matembezi hayo yanatajwa kama sehemu ya msingi katika kuendeleza umoja na mshikamano siyo tu miongoni mwa vyombo vya ulizni na usalama  bali pia mahusiano mema na jamii kwa maendeleo ya Mkoa wa Songwe.

Posted in

Leave a comment