
Na Cartace Ngajiro
Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Mizengo Pinda amewaasa wafanyabiashara wa mazao ya kilimo nchini kutumia Bandari ya Tanga kusafirsha mazao yao kwenda kwenye Soko la Kimataifa.
Pinda aliyasema hayo wakati wa ufunguzi wa Maonesho ya Nanenae Kanda ya Mashariki 2025, yanayojumuisha Mikoa minne Tanga, Dar es Salama, Pwani na Morogoro yanayofanyika katika Uwanja wa Mwalimu JK Nyerere maarufu kama ‘Viwanja vya NaneNane’
“Bandari ya Tanga inatupa heshima sana katika nchi yetu hivyo natoa rai kwa wafanyabiashara wa mazao ya kilimo nchini kutumia Bandari hiyo ambayo imeboresha huduma zake” aliongeza Mhe Pinda
Aidha alitoa wito kwa Shirika la Reli la Tanzania (TRC) na Bandari ya Tanga kuendelea kushirikiana ili kupanua wigo katika utoaji wa huduma katika sekta ya usafirishaji chini kanda ya mashariki.

Maonesho ya NaneNane Kanda ya Mashariki, 2025 yanayoshirikisha taasisi za umma na binafsi na Bandari ya Tanga ni mshiriki wa maonesho hayo yenye kauli mbiu ya ‘Chagua Viongozi Bora kwa Maendeleo Endelevu ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi 2025’

Leave a comment