
Na Mack Francis-Arusha
Serikali imetoa shilingi bilioni 139 kwa mikoa ya Arusha, Kilimanjaro na Manyara kwa ajili ya kuwezesha utekelezaji wa miundombinu ya kilimo cha umwagiliaji, ikiwa ni jitihada za kuwaondoa wakulima kwenye kilimo cha kutegemea mvua.
Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Queen Sendiga aliyaema hayo wakati akifungua Maonesho ya 31 ya Kilimo na Ufugaji Kanda ya Kaskazini, yanayoendelea katika viwanja vya Themi, mkoani Arusha, Agosti 5, 2025.
Alieleza kuwa sehemu ya fedha hizo ni matokeo ya ongezeko la bajeti ya taifa kwa ajili ya umwagiliaji, ambapo imeongezeka kutoka bilioni 46 mwaka 2021/2022 hadi kufikia bilioni 403.
“Ongezeko hilo limechangia kuzalishwa kwa mazao mbalimbali nchini kwa wingi, hivyo kuongeza usalama wa chakula na mauzo ya bidhaa za kilimo nje ya nchi”, alisema Sendiga.

Leave a comment