Na Damasi Kalembwe

Mkuu wa Ushirikishwaji wa Jamii Mkoa wa Kinondoni, ACP Ally Wendo amezindua kituo cha polisi kinachohamishika cha Kuzidi maeneo ya Goba, Kinzudi jijini Dar es salaam.

Uzinduzi huo ulifanyika juzi na ulihudhuriwa na  maafisa wa jeshi hilo, wakaguzi, askari wa vyeo mbalimbali, viongozi wa serikali ya mtaa  na wananchi wa mtaa huo.

Katika uzinduzi huo, wananchi walipewa elimu ya ukatili wa kijinsia, aina zake, namna ya kutanzua uhalifu, kuanzisha vikundi vya ulinzi shirikishi katika mItaa, kuchangia pesa ya ulinzi pamoja na  kutoa taarifa za wahalifu na uhalifu.

Katika hatua nyingine, ACP Wendo ameupongeza uongozi wa serikali ya mtaa wa Kinzudi na wananchi kwa ushirikiano uliofanikisha kukamilika kwa kituo hicho kidogo cha polisi.

ACP Wendo alifanya uzinduzi huo kwa niaba ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni SACP Mtatiro Kitikwi na aliwataka wananchi kuendelea kushirikiana na jeshi la polisi na kuwapa ushirikiano askari watakaopangiwa majukumu katika kituo hicho.

Posted in

Leave a comment