Na Damasi Kalembwe

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Acp Pili Misungwi amekabidhi pikipiki mbili kwa watendaji wa dawati la jinsia na watoto Wilaya ya Kimara na Kinondoni. Makabidhiano hayo yamefanyika leo katika kituo cha Polisi Oystebay ambapo yamehudhuriwa na maofisa, wakaguzi na askari wa vyeo mbalimbali Mkoa wa kinondoni.

Watendaji wa dawati la jinsia na watoto waliokabidhiwa pikipiki hizo wamepewa elimu  na matumizi sahihi ya vyombo hivyo ambvyo ni kwa ajili ya kuhakikisha wanawafikia wananchi kila eneo kwa haraka na kuwapatia huduma za kutanzua ukatili wa kijinsia.

Posted in

Leave a comment