
Na Damasi Kalembwe-Dar es Salaam
Shule ya Sekondari Saranga iliyopo Mtaa wa Matangini, Kata ya Saranga, imefanya mahafali ya kuhitimu Kidato cha Nne ambapo pamoja na sherehe hizo, wanafunzi na wazazi walipata elimu ya ushirikishwaji jamii kutoka Jeshi la Polisi.
Katika mahafali hayo, Polisi wa Kata ya Saranga Insp. Elias na Polisi wa Kata ya Kimara Insp. Mussa walihudhuria na kutoa mada kuhusu umuhimu wa kushirikiana na jamii katika kulinda usalama, kupinga vitendo vya uhalifu na kuimarisha maadili kwa vijana.

Sherehe hizo zilihudhuriwa na walimu wakuu wa shule za binafsi na za serikali za Kata ya Saranga, walimu na wafanyakazi wa shule, wazazi pamoja na wageni waalikwa huku mgeni rasmi alikuwa mwakilishi wa uongozi wa elimu kata hiyo.
Viongozi hao wa polisi walisisitiza kuwa elimu na nidhamu ni nguzo muhimu za maendeleo ya taifa na kuwataka wahitimu kutumia vyema maarifa waliyoyapata kwa faida yao na jamii inayowazunguka.

Leave a comment