Na Alvar Mwakyusa

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetangaza kuwa mvua zitaendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali ya nchi, hasa katika kanda ya Ziwa Victoria, magharibi mwa nchi, na nyanda za juu kusini-magharibi.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa, mvua zinazoambatana na ngurumo za radi zinatarajiwa katika maeneo machache ya kanda ya Ziwa Victoria, magharibi mwa nchi, na nyanda za juu kusini-magharibi.

Taarifa hiyo inatoa muhtasari wa mwenendo wa mvua kati ya Novemba 21 na 30 mwaka huu na matarajio ya mvua kwa Disemba 01 mpaka 10 mwaka huu.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo mikoa ya Kagera, Geita, Shinyanga, Mwanza, Simiyu, na Mara inatarajiwa kupata mvua zinazoambatana na ngurumo za radi katika kipindi cha siku tano za mwisho za tarehe tajwa.

Pia, mikoa ya Kigoma, Katavi, na Tabora inatarajiwa kupata mvua zinazoambatana na ngurumo za radi katika kipindi cha siku tano za mwisho.

Hali ya ukavu inatarajiwa katika mikoa ya Arusha, Manyara, na Kilimanjaro, pamoja na kanda ya kati (Dodoma na Singida).

Mamlaka ya Hali ya Hewa imetoa wito kwa wananchi kuchukua tahadhari na kufuatilia taarifa za hali ya hewa ili kujiandaa na mabadiliko ya hali ya hewa

Posted in

Leave a comment