Na Farida Mkumba

Wataalamu mbalimbali wa Bajeti kutoka Chuo cha Serikali za Mitaa wamekutana Jijini Dodoma na kufanya mapitio ya mpango mkakati wa Chuo hicho kuanzia 2026 hadi 2031.

Mafunzo hayo ya siku tano kuanzia Tarehe 06 hadi 09 Januari, 2026 yametolewa na Kurugenzi ya Mipango ya Mipango ya Chuo hicho ili kuwapa uelewa mpana wataalamu hao katika utekelezaji mipango kimkakati itakayoleta tija katika Chuo hicho.

Akifungua Mafunzo hayo, Mkuu wa Chuo hicho, Dkt.Yusuph Mashala amewataka wataalamu hao kufuatilia kwa umakini kwani mipango yote ya maendeleo itatokana na mpango mkakati huo.

Katika kuhakikisha Chuo cha Serikali za Mitaa kinakuwa na kuendelea kutoa huduma kwa umma kwa sasa kina kampasi tatu ambazo ni Kampasi Kuu Hombolo, Kampasi ya Shinyanga na Kampasi ya Dodoma Mjini na pia Chuo kimeshapata eneo Mkoani Njombe ili kuendelea kutoa huduma kwa kanda ya Nyanda za juu Kusini.

Posted in

Leave a comment