
Na Farida Mkumba
Wanafunzi wa Chuo cha Serikali za Mitaa Kampasi ya Shinyanga wametembelea Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Shinyanga kuwaona wagonjwa, kufanya usafi eneo lote linalozunguka Hospitali hiyo, kujitolea damu na kutoa misaada mbalimbali za Kijamii.
Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi wangonjwa na wananchi mbalimbali wameeleza namna wanavyoridhishwa na uwepo wa Chuo cha Serikali za Mitaa Mkoani Shinyanga kwa kuwa uwepo wake unadhihirika katika mambo mbalimbali yanayohusu jamii.
Pamoja na mambo mengine, wanafunzi hao wamechanga pesa na kwenda kuziona jamii zenye uhitaji na hii ni katika kuonesha kuwa pamoja na kujipatia elimu kama sehemu ya jamii wanashiriki shughuli mbalimbali za kijamii.

Kwa upande wa Maneja Kampasi wa Chuo hicho Mkoani Shinyanga Dkt.John Kasubi amesema kuwa Chuo kitaendelea kujitolea kwa Jamii ya Shinyanga kila kinapopata fursa katika maeneo mbalimbali ya Mkoa huo na kuwataka wananchi wakipe ushirikiano ili kuionesha Jamii kuwa mbali na utoaji wa elimu pia Chuo kinajitolea kuisaidia jamii inayokizunguka chuo hicho.

Leave a comment