Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Katika mwendelezo wa utoaji wa elimu kwa umma, Jeshi la polisi limeendelea na kazi hiyo ambapo jana, Mratibu wa Program ya Usalama Wetu Kwanza Wilaya ya Kati na Kariakoo Mkaguzi Msaidizi wa Polisi (Insp) Martin Shila alifika katika Shule ya Msingi Olympio Iliyopo Upanga Dar es salaam na kuzungumza na wanafunzi wa Shule hiyo.

Katika tukio hilo Insp Shilla aliwaeleza watoto hao kuwa kila mtu ana mchango katika kuzuia ukatili hivyo kuwataka kuwajibika katika kupambana na changamoto hiyo katika katika jamii.

Aidha katika hatua nyingine Insp Shilla alibainisha mazingira hatarishi yanayoweza kusababisha ukatili kutokea na kuwaasa kutoa taarifa katika vituo vya polisi, ofisi za serikali za mitaa na mamlaka nyingine za kisheria.

Posted in

Leave a comment