Na Mwandishi Wetu, Dar es salaam

Mkuu wa Polisi Jamii Wilaya ya Kariakoo Mrakibu wa Polisi (SP) Rosemary Kitwara amewataka wananchi kujiepusha na taarifa za upotoshaji zinazotolewa na watu mbalimbali wasio na mamlaka ya kutoa taarifa kwa jamii.

SP Kitwara aliyasema hayo jana wakati wakati akizungumza na wafanyabiashara wa Kariakoo Dar es salaam ambapo amewaasa kupuuza taarifa za uongo zinazosambazwa katika mitandao ya kijamii ambazo vyanzo vyake si sahahi na hivyo kusababisha taharuki katika jamii.

Pia amewaasa wafanyabiashara na wananchi kwa ujumla kutojihusisha na  uhalifu na kuwaomba kutoa taarifa za wahalifu uharifu ili kuzuia vitendo hivyo katika eneo hilo la biashara na sehemu zingine.

Posted in

Leave a comment