Na Cosmas Msuha

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule, ametembelea Banda la Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) wakati wa Maonesho ya Mafanikio ya Siku 100 za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Maonesho hayo yalifanyika jana, katika Uwanja wa Nyerere Square jijini Dodoma yakibeba kaulimbiu “Kero yako, wajibu wangu; Huduma Bora, Maisha Bora.”

Akiwa katika banda la WCF, Senyamule alipata maelezo kuhusu majukumu na huduma mbalimbali zinazotolewa na WCF, hususan katika kutoa fidia kwa wafanyakazi wanaopata ajali au magonjwa yatokanayo na kazi pamoja na juhudi za mfuko katika kuimarisha ustawi na usalama wa wafanyakazi nchini.

Aidha, ameupongeza mfuko huo kwa kuendelea kutoa elimu kwa wananchi na waajiri kuhusu umuhimu wa kujiunga na mfumo wa fidia kwa wafanyakazi, hatua inayochangia kulinda haki na maslahi ya wafanyakazi.

Sambamba na hayo amesisitiza umuhimu wa taasisi za umma na sekta binafsi kuhakikisha changamoto za wananchi zinapatiwa ufumbuzi kwa haraka ili kupunguza malalamiko na kuongeza ufanisi wa utoaji huduma.

Mh. Rosemary Senyamule akiwasili kwenye Maonesho ya Mafanikio ya siku 100 za Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan yaliyofanyika jana Nyerere square Dodoma (Picha na Mwandishi wetu).

Posted in

Leave a comment