Na Mwandishi Wetu, Dodoma

Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Nzuguni iliyopo jijini Dodoma wamepata fursa ya kujifunza na kufahamu huduma mbalimbali zinazotolewa na Chuo cha Serikali za Mitaa.

 Maelezo nae limu hiyo waliipata jana baada ya kutembelea banda la maonyesho la chuo hicho katika maadhimisho ya siku 100 za mafanikio ya serikali ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Katika maonyesho hayo, walipata maelezo kutoka kwa Afisa Uhusiano wa chuo, Leonard Maona kuhusu programu za masomo, mafunzo na huduma nyingine zinazotolewa kwa lengo la kuwajengea uwezo watumishi wa serikali za mitaa pamoja na vijana wanaotaka kujiendeleza kitaaluma katika sekta hiyo.

Maadhimisho ya siku 100 za mafanikio ya serikali yalifanyika katika viwanja vya Nyerere Square, jijini Dodoma, ambapo taasisi mbalimbali za serikali zilipata nafasi ya kuonesha shughuli na huduma wanazotoa kwa wananchi.

Maonesho hayo yalianza rasmi tarehe 4 Machi 2026 na kuhitimishwa jana yakilenga kuwapa wananchi nafasi ya kujionea mafanikio yaliyopatikana ndani ya siku 100 pamoja na kupata elimu kuhusu huduma za taasisi mbalimbali za umma.

Posted in

Leave a comment