Kusini Kwetu
Habari za ndani na nje nchi
recent posts
- TAKUKURU Kuendelea Kufuatilia, Kuthibiti Matumizi Fedha za Miradi ya Serikali
- BARIKIWA NA NYIMBO ZA KWARESMA
- Kukamilika Soko la Samaki Kutaibua Fursa za Uchumi, Ajira kwa Wananchi
- DC Moyo Agawa Miche ya Mikorosho kwa Wakulima Nachingwea
- Mt. Kizito Makuburi – Buriani Baba Pengo (Official Music Video)
about
Category: Uncategorized
-
Na Mwandishi Wetu Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Ally Ussi amempongeza Waziri wa Fedha Dkt. Mwigulu Nchemba kwa usimamizi madhubuti na utoaji wa fedha katika miradi mbalimbali ya maendeleo nchini. Ussi alitoa pongezi hizo wakati wa ukaguzi na uwekaji wa jiwe la msingi katika ujenzi wa daraja la Konkilangi na barabara ya…
-
Na Issa Mwadangala. Madereva wa vyombo vya moto wanaofanya safari zao Barabara ya Mbeya-Tunduma wametakiwa kuacha tabia ya kuendesha vyombo hivyo kwa mazoea ili kupunguza ajali za barabarani. Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Raphael Magoma aliyasema hayo jana wakati akitoa elimu kwa madereva na abiria katika eneo la ukaguzi wa magari lililopo Chimbuya Wilaya ya Mbozi…
-
Na Vincent Mpepo Vijana wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Mtaa wa Kwembe wameelezea mafanikio, fursa na changamoto zinazowakabili katika safari ya kujikwamua kichumi kama sehemu ya jamii huku wakitoa rai kwa washarika na jamii kuwaunga mkono katika harakati zao. Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa Vijana Mtaani hapo, Abel Mvungi Siku ya Jumapili…
-
Wimbo maalum kwa ajili ya kumpa heshima Mt. Yosefu. Ni wa kusikiliza (Audio), kutafakari, na kuomba ulinzi wa Mt. Yosefu. Furahia kazi ya sanaa kutoka kwa Wanakwaya wa Kwaya ya Damu Takatifu ya Yesu, Tegeta, Dar es Salaam, Tanzania.
-
Na Vincent Mpepo Makamu Mkuu wa chuo Kikuu Huria cha Tanzania, Profesa Alex Makulilo amewataka wafanyakazi wa chuo hicho kubadilika kifikra na kiutendaji ili kuendana na ushindani katika mifumo ya uendeshaji taasisi za elimu ya juu kutoka ndani na nje ya nchi. Profesa Makulilo alitoa wito huo jana wakati wa mkutano wake wa kwanza na…
-
Na Mwandishi Wetu Mtangazaji mstaafu wa Redio Tanzania Dar es Salaam (RTD), Edda Sanga, ameelezea kukerwa na utangazaji wa mzaha na ucheshi unaovunja miiko ya tasnia hiyo kwa kuwa madai kuwa studio ni eneo la kuheshimiwa sio kupiga kelele au kurushiana maneno. Sanga alitoa kauli hiyo jana wakati wa mafunzo kwa watangazaji chipukizi kutoka vyuo…
-
Na Vincent Mpepo Watangazaji wakongwe wa iliyokuwa Redio Tanzania Dar es salaam (RTD) ambayo kwa sasa ni sehemu ya Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) wametumia siku ya maadhimisho ya miaka 74 ya utangazaji Tanzania kubalishana uzoefu na waandishi wa habari watangazaji chipukizi ili kuhakikisha wanarithisha amali njema katika tasnia ya hiyo. Wakizungumza wakati wa mafunzo…
-
Na Vincent Mpepo Wanawake walio kwenye ndoa wametakiwa kuwasaidia waume zao katika majukumu ya kifamilia kwa kufanya kazi badala ya kuwa wategemezi na walalamishi ili kuwapunguzia msongo wa mawazo na vifo waume zao. Kauli hiyo imetolewa jana na Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Kiinjili Kilutheri Tanzania (KKKT), Ismail Mwipile wa Usharika wa Segerea jijini Dar…
-
Na Tabia Mchakama Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) imeshuhudia ulipwaji wa fidia kwa Bi. Bahati Ngowi kufuatia kufuatia kifo cha mume wake Profesa Ngowi aliyepata ajali ya gari maeneo ya Mlandizi Kibaha mkoani Pwani tarehe 28 Machi 2022. Akishuhudia tukio hilo Kamishna wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania, Dkt. Baghayo Saqware alizitaka…