Na Vincent Mpepo, Morogoro

Mkuu wa Kitivo cha Sanaa na Sayansi za Jamii cha Chuo Kikuu Huria cha Tanzania amewashukuru wafanyakazi wawakilishi wa idara za kitivo hicho na kuwataka kuendelea kufanya kazi kwa bidii kwa manufaa ya idara, kitivo na chuo kwa ujumla.

Mtiva, Dunlop Ochieng alitoa kauli hiyo juzi Mjini Morogoro wakati akifungua kikao kazi kwa wawakilishi wa idara mbalimbali za kitivo hicho huku wito wake ni kuwataka kuendelea kufanya kazi kwa juhudi na maarifa.

 “Nawashukuru kwa kuja na kuendelea kufanya kazi licha ya changamoto mbalimbali”, alisema Mtiva Ochieng.

Aidha alisema kumekuwa na changamoto katika nyaraka za kitivo na chuo ambazo zina maelekezo na gharama ambazo zinatofatiana kitu ambacho inabidi wawakilishi hao wakifanyie kazi ili kuwa na taarifa sahihi na za uhakika.

Mratibu wa Uwasilishaji tafiti wa Kitivo hicho, Dkt. Ladisalus Batinoluho alimshukuru Mtiva kwa kuwaamini na kuwapa jukumu hilo na kwamba hawatamuangusha ili kuhakikisha kazi hiyo inafanyika kwa weledi.

“Hata kama kutakuwa na marekebisho tupo tayari kuyafanya ili mwisho wa siku malengo ya kazi hii yafikiwe”, alisema Dtk.Batinoluho.

Mwakilishi wa Kitengo cha Udhibiti Ubora cha Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, Mhadhiri Msaidizi Janeth Gwimile aliema anashukuru kitivo hicho kwa kuonesha njia ya kuhakikisha kunakuwa na taarifa za uhakika na kwamba kitengo chake kushirikishwa ni jambo muhimu kwa kuwa kimekuwa kikisisitiza masuala ubora kama sehemu ya majukumu yake.

Kwa upande wake, Mhadhiri Emmanuel Msangi alimshukuru Mtiva kwa uamuzi wake na kwamba wapo tayari kuendelea kujifunza ili kuhakikisha kila kitu kinafanyika kwa ubora.

Mtaalamu wa Usanifu wa maandishi na machapisho, Thomas Kilumbi alisema kitivo hicho kimeonseha njia kwa kumshirikisha katika hatua za awali ambapo anaweza kufanya kazi hizo kwa kushirikiana na wahusika na kujua mahaitaji yao na wakati mwingine kushauri namna bora zaidi.

Posted in

3 responses to “Mtiva Awashukuru kwa Kazi Nzuri”

  1. Emmanuel Msangi avatar
    Emmanuel Msangi

    Bw. Mpepo, kongole Kwa jitihada hizi.

    Liked by 1 person

  2. Ochieng avatar
    Ochieng

    Hongera kwa kazi nzuri unayoifanya

    Liked by 1 person

    1. mpepovincentgmailcom avatar
      mpepovincentgmailcom

      Asante sana Mtiva

      Liked by 1 person

Leave a reply to Emmanuel Msangi Cancel reply