Na Vincent Mpepo

Wafanyakazi wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT) wametakiwa kuendelea kufanya kazi kwa bidii ili kuboresha utoaji wa huduma na kukuza mapato ya chuo hicho.

Makamu Mkuu wa Chuo, Profesa Alex Makulilo, alitoa wito huo jana katika hafla ya uzinduzi wa gari jipya la ofisi yake iliyofanyika Kinondoni, jijini Dar es Salaam.

Alisema menejimenti ya chuo inaendelea kuboresha mazingira ya kazi kadiri uwezo wa kifedha unavyoruhusu.

“Natambua kuna mahitaji mengi ikiwemo samani na vitendea kazi vingine, lakini tutajitahidi kuboresha mazingira ya kazi kulingana na uwezo wetu,” alisema Profesa Makulilo.

Aidha, alilipongeza kila kitengo kilichohusika katika mchakato wa ununuzi wa gari hilo na kubainisha kuwa fedha zilizotumika zimetokana na mapato ya ndani ya chuo.

Kwa upande wake, Naibu Makamu Mkuu wa Chuo anayeshughulikia Huduma za Mikoa na Teknolojia za Kujifunzia, Profesa Leonard Fweja, alisema kuwa gari hilo limekuja kwa wakati muafaka, na litasaidia kuboresha usafiri wa kiongozi huyo katika kutekeleza majukumu mbalimbali, ikiwemo kuvifikia vituo vya mikoa vya chuo hicho mikoani.

Naye Kaimu Naibu Makamu Mkuu wa Chuo anayeshughulikia Masuala ya Taaluma, Utafiti na Ushauri wa Kitaalamu, ambaye pia ni Mkuu wa Kitivo cha Sanaa na Sayansi za Jamii, Dkt. Dunlop Ochieng, alisema kuwa upatikanaji wa gari hilo ni matokeo ya kufanya kazi kwa bidii.

“Haya ni matunda ya juhudi za pamoja na ninawaomba wafanyakazi wenzangu tuendelee kujituma kwa sababu kufanya kazi kwa bidii kunalipa,” alisema Dkt. Ochieng.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Mipango na Maendeleo wa Chuo, Benjamin Bussu, alisema mchakato wa ununuzi wa gari hilo ulianza Februari 2025 na umefuata taratibu zote, ikiwemo kuomba kibali kwa Katibu Mkuu Kiongozi, kwa kuwa chuo kilihitaji gari linaloendana na hadhi ya taasisi na kiongozi wake.

“Ninatoa rai kwa madereva kulitunza gari hili na kulitumia kwa uangalifu ili kuhakikisha usalama wa viongozi,” alisema Bussu.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi huyo, gari lililonunuliwa ni Toyota Land Cruiser, ambalo limegharimu kiasi cha shilingi milioni 386.

Uzinduzi wa gari hilo ulitanguliwa na dua, sala na maombi kutoka kwa watumishi mbalimbalimbali chuoni hapo ikiwemo mhadhiri Msaidizi na Mchungaji Hanington Kabuta, Mkurugenzi wa Rasilimali watu wa chuo hicho Francis Badundwa na Dtk. Omari Mohamed suala linalodhihirisha imani na heshima kwa Mungu wakitambua kuwa kila kitu kiafanyika kwa uwezo wa Mungu.

Posted in

One response to “Wakumbushwa Kuendelea Kufanya Kazi kwa Bidii”

  1. psychicreallyb3855347c2 avatar
    psychicreallyb3855347c2

    Sawa

    Like

Leave a reply to psychicreallyb3855347c2 Cancel reply