
Na Juma John Elisha
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Deogratius Ndejembi, ameapishwa rasmi kushika wadhifa huo katika hafla iliyofanyika Ikulu ya Chamwino, Dodoma.
Ndejembi ameapa mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, na hivyo kuanza rasmi majukumu yake mapya kama Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Uteuzi wa Ndejembi umefuatia kuondoka kwa aliyekuwa Makamu wa Rais, Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, ambaye alijiuzulu nafasi hiyo Agosti 25, 2026. Hatua hiyo ilisababisha kuwepo kwa nafasi wazi na kufungua mchakato wa kumpata Makamu wa Rais mpya.
Hafla ya kuapishwa kwa Ndejembi imefanyika katika Ikulu ya Chamwino, Dodoma, ikiashiria mwanzo rasmi wa utekelezaji wa majukumu yake katika nafasi hiyo muhimu ya uongozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Ndejembi anatarajiwa kushirikiana kwa karibu na Rais Samia Suluhu Hassan katika utekelezaji wa majukumu ya Serikali, ikiwemo kusimamia maeneo atakayokabidhiwa kwa mujibu wa Katiba na sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Leave a comment