
Happy Milion
Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi linamshikilia Josephina Mbizimungu (30), mkazi wa Kijiji cha Kapalala, kwa tuhuma za kumjeruhi mtoto wake wa kiume mwenye umri wa siku nne kwa kumkata sehemu za siri.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Kaster Konyani, amesema tukio hilo lilitokea Oktoba 25, 2026, saa 3:00 asubuhi. Tukio hilo liligundulika wakati bibi wa mtoto huyo alipokuwa akimuogesha na kubaini kuwa sehemu zake za siri zilikuwa zimekatwa.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, uchunguzi wa awali umebaini kuwa mtuhumiwa anadaiwa kuwa na changamoto za afya ya akili. Kufuatia tukio hilo, mtoto huyo alipelekwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi kwa ajili ya kupatiwa matibabu, huku hali yake ikiendelea kuimarika.
Jeshi la Polisi limewataka wazazi na walezi kuwalinda watoto dhidi ya vitendo vya ukatili na unyanyasaji, likisisitiza kuwa wana wajibu wa kuhakikisha usalama na ustawi wao.

Leave a Reply