Na Mwandishi Wetu

Watahiniwa 429,667 sawa na asilimia 37.72 ya watahiniwa waliofanya Mtihani wa Kumaliza Elimu ya Msingi (Darasa la Saba) mwaka 2026 wamepata madaraja ya juu ya A na B.

Idadi hiyo imeongezeka kwa asilimia 0.82 ikilinganishwa na matokeo ya mwaka 2025.

Akizungumza wakati akitangaza matokeo hayo leo, Novemba 3, 2026, Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA), Profesa Said Mohamed, amesema jumla ya watahiniwa 970,876 sawa na asilimia 85.22 ya watahiniwa 1,139,273 waliofanya mtihani huo wamefaulu kwa kupata madaraja ya A, B na C.

Amesema kiwango hicho cha ufaulu kimeongezeka kwa asilimia 3.42 ikilinganishwa na mwaka 2025, ambapo ufaulu ulikuwa asilimia 81.80.

Posted in

Leave a Reply