Category: Uncategorized

  • Na Pilastus Nyaulingo Tanzania inakabiliwa na changamoto katika kufikia malengo ya kuongeza matumizi ya nishati safi ya kupikia, huku gharama za nishati, upatikanaji wa teknolojia na utekelezaji wa sera zikitajwa kuwa miongoni mwa mambo yanayohitaji kupewa kipaumbele. Wakizungumza kuhusu utekelezaji wa mpango wa Tanzania wa kuongeza matumizi ya nishati safi ya kupikia, wadau wa nishati…

  • Na George Gabriel Waziri wa Viwanda na Biashara, Judith Kapinga, amekipongeza Kikundi cha Vijana Kazi Imara cha Kata ya Nanyumbu, Wilaya ya Nanyumbu, kwa uaminifu katika marejesho ya mikopo, ubunifu na ubora wa bidhaa wanazozalisha. Kapinga alitoa pongezi hizo jana wakati wa ziara yake wilayani Nanyumbu, ambapo alikagua shughuli mbalimbali zinazofanywa na vijana hao, ikiwemo…

  • Na Pilastus Nyaulingo Wataalamu wa teknolojia ya habari na mawasiliano wameitaka Tanzania kuimarisha imani ya wananchi katika huduma za kidijitali, ikiwemo usalama wa mtandao, ulinzi wa taarifa binafsi na ujuzi wa kidijitali, ili nchi iweze kunufaika zaidi na teknolojia ya akili bandia (AI) na uchumi wa kidijitali. Wito huo umetolewa katika Jukwaa la Tanzania Digital…

  • Na Yusra Temba Mlimbwende Jihan Dimack ameibuka mshindi wa taji la Miss Grand Tanzania 2026, baada ya kuwashinda washiriki wengine kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania katika shindano lililojumuisha vipengele vya mahojiano, mawasilisho, matembezi ya jukwaani na uwezo wa kujieleza mbele ya majaji na hadhira. Ushindi huo ulishuhudiwa na wadau mbalimbali wa tasnia ya burudani, urembo na…

  • Na Juma John Elisha Usajili wa mshambuliaji wa Kitanzania, Selemani Mwalimu “Gomez”, kwenda Yanga SC umegeuka kuwa moja ya habari kubwa katika dirisha la usajili kuelekea msimu wa 2026/27, hasa kutokana na namna ulivyokuja baada ya Simba SC kuwahakikishia mashabiki wake kuwa mchezaji huyo angeendelea kuitumikia klabu hiyo. Yanga imemtambulisha rasmi Mwalimu kuwa mchezaji wake…

  • Na Pilastus Nyaulingo, Tanga Wito umetolewa kwa madereva wa bodaboda nchini kuongeza tahadhari wanapopokea abiria, hasa wanaowaomba safari za umbali mrefu, kufuatia kifo cha dereva mwenye umri wa miaka 18, Rajab Arufan, aliyefariki baada ya kwenda katika safari ya Lukozi, Wilaya ya Lushoto. Rajab, aliyekuwa akifanya kazi katika kituo cha bodaboda Mabanda ya Papa jijini…

  • Na Pilastus Nyaulingo, Dodoma Wadau wa sekta ya kilimo na mazingira wameeleza kuwa kilimo mseto cha miti na mazao kinaweza kuwa fursa muhimu kwa vijana kujiajiri, kuongeza kipato na kuchangia kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabianchi. Kauli hiyo imetolewa katika mkutano wa wadau uliofanyika Dodoma, pembezoni mwa maonesho ya Nane Nane, ambapo washiriki walijadili…

  • Na Pilastus Nyaulingo, Ushetu, Shinyanga Halmashauri ya Ushetu kupitia Idara ya Elimu imemkabidhi Tuzo ya Heshima Mbunge wa Jimbo la Ushetu, Emmanuel Cherehani, kwa kutambua mchango wake katika kuimarisha sekta ya elimu na kuunga mkono juhudi za kuboresha huduma za elimu katika halmashauri hiyo. Tuzo hiyo ilikabidhiwa jana katika hafla iliyosisitiza umuhimu wa ushirikiano kati…

  • Na Pilastus Nyaulingo Mradi wa Mabasi yaendayo Haraka (BRT) Awamu ya Pili unatarajiwa kuboresha huduma za usafiri wa umma kwa wakazi wa Dar es Salaam na kusaidia kupunguza gharama za safari kwa wananchi. Kauli hiyo ilitolewa jana wakati wa uzinduzi wa mradi huo jijini Dar es Salaam, ambapo viongozi walisema BRT Awamu ya Pili ni…

  • Na Pilastus Nyaulingo Wadau wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) wameitaka Serikali kutambua kisheria mitandao ya jamii ya mawasiliano kama watoa huduma za kidijitali zisizo za kibiashara, wakisema hatua hiyo inaweza kusaidia kuongeza upatikanaji wa intaneti katika maeneo ya vijijini na yaliyo pembezoni. Wito huo umetolewa hivi karibuni jijini Dar es Salaam na wadau…