Category: Uncategorized
-
Na Juma John Elisha Dar es Salaam — Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu, amesema atatumia haki yake ya kujitetea mwenyewe katika kesi ya uhaini inayomkabili, baada ya Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam, kuamua kuwa ana kesi ya kujibu. Uamuzi huo umetolewa leo, Agosti 21, 2026, na…
-
Na Pilastus Nyaulingo Wanaishi nyumba moja. Wanalala kitanda kimoja. Wanaweza hata kula chakula mezani pamoja. Lakini wakati mwingine au wakati wote, kila mmoja anaishi katika dunia yake. Mmoja anashika simu kuangalia WhatsApp. Mwingine anaingia Instagram, TikTok au Facebook. Dakika zinapita, saa zinapita, siku zinapita mazungumzo yanapungua na ukimya unatawala. Kwa nje, ndoa inaonekana na kila kitu…
-
Na Pilastus Nyaulingo Nyumbani kunaweza kuwa na watu wengi, lakini mazungumzo yakawa machache. Mzazi anaweza kuwa ameketi kwenye kiti akijibu ujumbe wa simu, mtoto akiwa upande mwingine akiangalia video na mwingine akicheza mchezo wa mtandaoni, huku muda ambao familia ingeutumia kuzungumza ukipita. Hii ndiyo hali mpya ambayo teknolojia imeleta ndani ya familia nyingi. Simu zimechukua…
-
Na George Gabriel Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu, Christopher Magala, amefungua mafunzo ya siku moja kwa madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu, yenye lengo la kuwajengea uwezo katika kutekeleza majukumu yao, hususan usimamizi wa fedha na rasilimali za umma. Akizungumza katika mafunzo hayo yaliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri, Magala alisema madiwani wana…
-
Na Pilastus Nyaulingo Mtoto wa kiume anapokua, mara nyingi huanza kufundishwa mapema kwamba siku moja atakuwa mwanaume wa familia. Anaambiwa anatakiwa kuwa jasiri, kufanya kazi, kujitegemea na kuhakikisha familia yake haikosi mahitaji muhimu. Lakini katika dunia inayobadilika, swali linabaki: Je, hayo ndiyo maandalizi yote anayohitaji mtoto wa kiume kabla hajawa mume na baba? Kuwa mwanaume…
-
Na Alex Msumeno Kamanda wa Kikosi cha Kuzuia Wizi wa Mifugo nchini, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Simon Pasua, amewataka viongozi wa kimila kuwa wasuluhishi wa migogoro katika jamii zao na kushirikiana na Jeshi la Polisi katika kuzuia migogoro baina ya wakulima na wafugaji. Wito huo umetolewa leo katika mnada wa mifugo uliopo Kata…
-
Waziri Saidi, Tabora Mkuu wa Polisi Jamii wa Tabora Manispaa, SP Honorata Oisso, amewaongoza maafisa na wakaguzi wa Jeshi la Polisi katika hafla ya kumuaga na kumpongeza Mkaguzi Mstaafu Hassara Mkobela. Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Tabora Manispaa jana katika Bwalo la Polisi, SP Novatus Nyabenda, ambaye pia ni Mkuu wa…
-
Na George Gabriel Wananchi wa Kijiji cha Mkuula, Wilaya ya Nanyumbu mkoani Mtwara, wameeleza kufurahishwa na mpango wa ujenzi wa mnara wa redio wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), wakisema mradi huo utawasaidia kupata taarifa mbalimbali za kitaifa na kijamii pamoja na burudani kwa wakati. TBC, kwa kushirikiana na Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF),…
-
Na Pilastus Nyaulingo Kwa mwanafunzi anayekaa darasani siku nzima, kengele ya mwisho inapolia inaweza kumaanisha mwisho wa masomo. Lakini kwa baadhi ya watoto wanaoishi katika maeneo ambayo upatikanaji wa umeme bado ni changamoto, mwisho wa vipindi vya darasani unaweza pia kumaanisha mwisho wa nafasi ya kujisomea kwa siku hiyo. Hii ni kwa sababu elimu haishii…
-
Na Andrea Mbona, Mbulu Matumizi ya pombe miongoni mwa waendesha bodaboda yameelezwa kuwa miongoni mwa sababu zinazochangia ajali za barabarani, huku madereva wakitakiwa kuepuka ulevi hasa wanapokuwa kazini. Askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani wilayani Mbulu, Cpl Octavian, ametoa rai hiyo wakati akitoa elimu ya usalama barabarani kwa waendesha bodaboda katika eneo la stendi ya…