Category: Uncategorized
-
Na Andrea Mbona, Mbulu Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Manyara, Mrakibu wa Polisi Mikael Mwakasungura, ametembelea Wilaya ya Mbulu na kufanya kikao cha kazi na askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani wa wilaya hiyo, akiwakumbusha wajibu wao wa kusimamia sheria za usalama barabarani kwa weledi na uadilifu. Akizungumza katika kikao hicho, Mrakibu…
-
Na Damasi Kalembwe Jeshi la Polisi, kupitia Mkuu wa Polisi Jamii Wilaya ya Kinondoni, SP Edna Maro, limetoa elimu ya usalama kwa wafanyakazi wa Hoteli ya Golden Tulip iliyopo Masaki, Dar es Salaam, likiwataka kutambua kuwa kila mmoja ana wajibu wa kulinda mali za hoteli na kutekeleza majukumu yake kwa weledi huku akiepuka kujihusisha na…
-
Na Damasi Kalembwe Mashindano ya michezo ya Polisi Jamii Cup katika Mkoa wa Kinondoni yamezinduliwa rasmi Julai 27, 2026, katika viwanja vya michezo vya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM). Uzinduzi huo ulihudhuriwa na Mgeni Rasmi, Mkuu wa Ushirikishwaji wa Jamii Mkoa wa Kinondoni, ACP Ally Wendo, aliyeambatana na Wakuu wa Himaya za Kinondoni…
-
Na Jastini Bukebuke Walimu wa Shule ya Msingi Simbaguji, iliyopo Kata ya Kanyala, Wilaya ya Geita, wametakiwa kuimarisha usimamizi wa vilabu vya kupinga ukatili wa kijinsia shuleni ili viendelee kuwajengea wanafunzi uelewa wa haki zao, ujasiri wa kutoa taarifa, maadili mema na uwezo wa kujilinda dhidi ya ukatili pamoja na vitendo vingine vinavyohatarisha usalama wao.…
-
Na George Gabriel Wananchi wa Kijiji cha Masugulu, Wilaya ya Nanyumbu mkoani Mtwara, wameiomba Serikali kuhakikisha Mradi wa Maji wa Mto Ruvuma–Mangaka unakamilika kwa wakati ili waanze kunufaika na huduma ya maji safi na salama. Akizungumza kwa niaba ya wananchi, Mwanahawa Juma alisema licha ya mradi huo kuanza kutekelezwa, bado wanaiomba Serikali kuongeza kasi ya…
-
Na Cosmas Msuha Zaidi ya shilingi bilioni 38 zimetumika kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo katika Wilaya ya Kongwa, mkoani Dodoma, katika mwaka wa fedha 2025/2026, huku Serikali ikiahidi kuendelea kuboresha huduma za elimu, afya, maji, mawasiliano na miundombinu. Hayo yameelezwa hivi karibuni na Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Angellah Kairuki, wakati wa mkutano…
-
Na Jastini Bukebuke Mkuu wa Kituo cha Polisi Kasamwa, Inspekta Said Juma, akishirikiana na askari wa kituo hicho, wamewafariji wagonjwa wanaopatiwa matibabu katika Kituo cha Afya Kasamwa kwa kuwapa pole na kuwakabidhi mahitaji muhimu. Tukio hilo lilifanyika Julai 25, 2026, katika Kituo cha Afya Kasamwa, Wilaya ya Geita, ikiwa ni sehemu ya jitihada za Jeshi…
-
Na Damasi Kalembwe Jeshi la Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni limewataka wamiliki wote wa vyombo vya moto kujitokeza kuhakiki magari yao na kuzingatia taratibu za usalama barabarani, likisisitiza kuwa kampeni ya “Nenda kwa Usalama” inalenga kupunguza ajali na kulinda maisha ya watumiaji wote wa barabara. Zoezi hilo linafanyika katika Kituo cha Polisi Oysterbay cha Zamani kuanzia Julai…
-
Na George Gabriel Wananchi wa Kata ya Nanyumbu wamepongeza ziara ya Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu, Christopher Magala, wakisema imeleta manufaa makubwa kwa jamii kupitia usikilizaji wa kero, utatuzi wa migogoro ya wakulima na wafugaji pamoja na usimamizi wa ugawaji wa pembejeo za kilimo kwa wakati. Wakizungumza baada ya kukamilika kwa ziara hiyo, wananchi walisema…