Category: Uncategorized
-
Na Cosmas Msuha Ofisi ya Waziri Mkuu imewawezesha watu wenye ulemavu kushiriki katika Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba) kupitia Shirikisho la Vyama vya Watu Wenye Ulemavu Tanzania (SHIVYAWATA). Ushiriki huo umewawezesha kuonesha bidhaa na huduma mbalimbali wanazozalisha na kuzitoa, pamoja na kufanya biashara katika Viwanja vya Mwalimu Julius…
-
Na George Gabriel, Mtwara Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Mtwara imetoa msaada wa vifaa mbalimbali kwa Hospitali ya Mangaka iliyopo Wilaya ya Nanyumbu, mkoani Mtwara, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa wajibu wake kwa jamii na kuunga mkono jitihada za Serikali katika kuboresha huduma za afya. Akizungumza wakati wa makabidhiano…
-
Na Yusra Temba, Iringa Msimu wa tano wa Great Ruaha Marathon umefanyika ndani ya Hifadhi ya Taifa Ruaha ukilenga kuhamasisha uhifadhi wa mazingira na kukuza utalii wa michezo. Mgeni rasmi katika hafla hiyo alikuwa Msajili wa Hazina na mlezi wa Great Ruaha Marathon, Nehemiah Mchechu, ambaye alimwakilisha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania…
-
Na Cosmas Msuha Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) imeshiriki Jukwaa la Biashara lililofanyika sambamba na Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba), kwa lengo la kutangaza fursa za uwekezaji, biashara na kuimarisha ushirikiano na wadau mbalimbali wa sekta ya madini. Jukwaa hilo limewakutanisha wafanyabiashara, wawekezaji na…
-
Na Jastini Bukebuke Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Geita, kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi pamoja na watumishi kutoka idara mbalimbali za serikali, limeendesha msako maalum wa ukaguzi wa miundombinu ya umeme katika Mtaa wa Mwambageni, Kata ya Nyarugusu, Wilaya ya Geita. Akizungumza wakati wa msako huo, Afisa Uendeshaji wa TANESCO Mkoa wa…
-
Na Mwandishi Wetu Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Nchemba, amewataka Watanzania kuendelea kudumisha amani na kutopuuza viashiria vya uvunjifu wa amani, akisisitiza kuwa vinaweza kuchafua taswira ya taifa. Dkt. Nchemba alitoa wito huo jana wakati wa ibada maalumu ya kilele cha harambee iliyofanyika Usharika wa Amani, mjini Singida, katika Kanisa…
-
Na Cosmas Msuha Serikali ya Tanzania imeingia makubaliano na kampuni mbili kutoka Japan ili kufungua fursa za soko la biashara ya kaboni kupitia Mpango wa Uratibu wa Pamoja wa Mikopo (JCM). Akizungumza wakati wa hafla ya utiaji saini wa makubaliano hayo iliyofanyika Juni 25, 2026, jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu…
-
Na Jastini Bukebuke Mtandao wa Polisi Wanawake Mkoa wa Geita (TPF-NET) umetembelea na kutoa msaada katika Kituo cha Kulelea Watoto Yatima cha Bin Ghanimu kilichopo Bwanga, Wilaya ya Chato, ikiwa ni sehemu ya juhudi zake za kuwafariji na kusaidia watoto wenye uhitaji katika jamii. Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Mkuu wa Kituo cha Polisi Bwanga,…
-
Na Cosmas Msuha Wananchi wa Kimara, Wilaya ya Ubungo jijini Dar es Salaam, wanatarajia kuondokana na changamoto za usafiri baada ya ujenzi wa Barabara ya TRA–King’ong’o unaoendelea kwa kiwango cha zege kufikia hatua nzuri. Hayo yalisemwa na Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano kwa Umma wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA),…