Category: Uncategorized

  • Na Jastini Bukebuke, Geita Mkaguzi wa Polisi Kata ya Nyakafulu, INSP Denis Rwehumbiza, amewataka wanafunzi kutovumilia wala kuficha vitendo vya ukatili wanavyofanyiwa nyumbani au shuleni, badala yake watoe taarifa kwa walimu, wazazi, viongozi wa maeneo yao au Jeshi la Polisi ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa dhidi ya wahusika. Rai hiyo ameitoa leo alipokuwa akitoa…

  • Na Jastini Bukebuke, Geita Afisa Tawala wa Wilaya ya Geita, Lucy Beda, kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Geita, Hashimu Komba, amefunga rasmi hafla ya kuwaaga wajumbe 15 wanaotarajia kupanda Mlima Kilimanjaro kupitia programu ya GGML Kili Challenge, inayofadhiliwa na Kampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML). Akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika jana, Beda…

  • Na Jastini Bukebuke Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita limemfikisha katika Mahakama ya Wilaya ya Chato, Lufuta Magoma (40), mganga wa kienyeji na mkazi wa Kijiji cha Rutunguru, akikabiliwa na shtaka la kumuua mama yake mzazi, Dotto Magoma Nyara (70). Mshtakiwa alipandishwa kizimbani jana, Julai 10, 2026, ambapo alisomewa shtaka la mauaji mbele ya Hakimu…

  • Na Cosmas Msuha Mjiolojia kutoka Ofisi ya Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Njombe, Abbas Mruma, amesema Tanzania inaendelea kujijengea nafasi muhimu duniani kutokana na kuwa na hifadhi kubwa ya madini ya kimkakati, yakiwemo graphite, lithium na rare earth elements, ambayo ni nguzo muhimu katika maendeleo ya teknolojia za kisasa na nishati safi. Mruma alitoa…

  • ‎Na Cosmas Msuha KAIMU Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino, Dkt. Sophia Nchimbi, kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, amezindua mradi wa Mama Tembe unaolenga kuhifadhi urithi wa kiutamaduni wa Wagogo, kuwawezesha wanawake na wasichana, pamoja na kukuza uchumi kupitia ubunifu wa asili. Uzinduzi wa mradi huo umefanyika hivi karibuni wilayani Chamwino, mkoani…

  • Na Cosmas Msuha WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), amemuapisha Massana Gibril Mwishawa kuwa Kamishna mpya wa Uhifadhi wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), akisema uteuzi wake unaashiria imani ya Serikali katika uwezo wake wa kuendeleza sekta ya uhifadhi na utalii nchini. Akizungumza katika hafla ya uapisho iliyofanyika jana katika…

  • Na Cosmas Msuha Wakazi wa Jiji la Dodoma wamesema ujenzi wa barabara za mzunguko umeleta manufaa makubwa kwao, ikiwemo kuongeza fursa za biashara, kurahisisha usafiri na kuchochea ukuaji wa uchumi katika maeneo yanayozunguka barabara hizo. Mmoja wa wakazi wa eneo la Nala, Bi. Minnael Msanga, alisema uwepo wa barabara hiyo umeongeza idadi ya watu wanaopita…

  • Na Cosmas Msuha Serikali imesema mageuzi yanayoendelea kutekelezwa katika sekta ya madini yameifanya Tanzania kuwa miongoni mwa nchi zenye mazingira bora ya uwekezaji barani Afrika, huku yakifungua fursa mbalimbali katika utafiti, uchimbaji, uchenjuaji, uchakataji na uongezaji thamani wa madini. Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa, alitoa kauli hiyo jana alipofungua Kongamano la Madini lililofanyika…

  • Na Cosmas Msuha Serikali imewaagiza wazalishaji wote nchini kutumia alama ya ‘Made in Tanzania’ ili kuongeza utambulisho na imani kwa bidhaa zinazozalishwa nchini, pamoja na kuimarisha ushindani wake katika masoko ya kimataifa. Agizo hilo limetolewa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Balozi Emmanuel Nchimbi, wakati wa kilele cha maadhimisho ya…