• Mkuu wa Idara ya Ustawi wa Jamii, Chuo Kikuu Huria cha Tanzania Dkt. Mariana Makuu akisisitiza jambo wakati wa kikao cha tathmini  ya kutekeleza program za kuwasaidia watu wenye ulemavu kikiwahusisha wadau mbalimbali wakiwemo, wahadhiri, walimu, maofisa maendeleo ya jamii na wafadhili kutoka nchini Norway iliyofanyika jijini Dar es salaam hivi karibuni katika ukumbi wa chuo hicho.

    Na Grace Mwakalinga, Dar es salaam

    Serikali imeshauriwa kuajiri wataalamu wa ustawi wa jamii kwenye  shule  za  msingi jumuishi  ili kuwahudumia kikamilifu watoto wenye mahitaji maalum ambao wakati mwingine hukosa  mtu wa karibu kujua mahitaji yao wawapo shuleni.

    Mapendekezo hayo yametolewa na Mkuu wa Idara ya Ustawi wa Jamii, Chuo Kikuu Huria cha Tanzania Dkt. Mariana Makuu wakati wa kikao cha tathmini  ya kutekeleza program za kuwasaidia watu wenye ulemavu kikiwahusisha wadau mbalimbali wakiwemo, wahadhiri, walimu, maofisa maendeleo ya jamii na wafadhili kutoka nchini Norway iliyofanyika jijini Dar es salaam hivi karibuni katika ukumbi wa chuo hicho.

    Alisema mahitaji ya matunzo kwa  watoto wenye mahitaji maalumu kwenye jamii na waliopo shuleni ni makubwa kutokana na kukithiri kwa vitendo vya ukatili wa kijinsia hivyo kuna uhitaji wa walimu kuongezewa nguvu kutoka kwa wataalamu wa ustawi wa jamii ambao watafanya kazi pamoja na walimu hao ili kuhahikisha ustawi wa watoto katika mazingira ya shule na jamii kwa ujumla.

    “Walimu peke yao hawawezi kwani wana majukumu ya  kutekeleza mtaala lakini hili la kuwasaidia kwa mambo mengine linaweza kufanyiwa kazi vyema na wataalamu wa ustawi wa jamii”, alisema Dtk. Makuu.

    Alisema kutokana na changamoto hiyo Chuo Kikuu Huria cha Tanzania kinaishauri serikali kuajiri wataalamu wa ustawi wa jamii kwenye shule zote jumuishi ili kuongeza nguvu ya kuwasaidia watoto hao kielimu, kiakili na kiafya ili  wawe sawa kama watoto wengine.

    “Idadi kubwa ya watoto wenye mahitaji maalum shuleni wanashindwa kutimiza ndoto zao kutokana na kukosa uangalizi maalum ili kusoma vizuri kama watoto wengine, alisema Dkt.Makuu.

    Mwalimu wa shule ya msingi jumuishi ya Uhuru Mchanganyiko, Catherine Chitanda, alisema utaratibu huo  utakuwa mwarobaini wa kuwasaidia watoto wenye mahitaji maalum shuleni kwa kupata usaidizi wa karibu kutoka kwa wataalamu wa ustawi wa jamii ambao watakuwepo shuleni kuwahudumia.

    Aidha Catherine alisema katika kufanikisha hilo, lazima serikali ikubali kushirikiana na jamii, walimu na wataalamu wa ustawi wa jamii ili kutimiza kikamilifu jukumu la  kuwatunza  na kuwalea watoto wenye mahitaji maalum shuleni.

    Mtalaam wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (ICT) Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, Stella Shayo, alisema katika kutekeleza programu hiyo chuo kimejipanga kutoa elimu juu ya ukatili wa kijinsia kwa wazazi, walezi na jamii juu ya athari za vitendo hivyo ili kuwaweka sawa kisaikolojia watoto hao wawapo shuleni.

    Kwa upande wake, Afisa Maendeleo ya Jamii Kata ya Kinondoni, Silider Ussuma alisema anaunga mkono jambo hilo na kwamba litasaidia kuwaweka sawa kiakili watoto wenye mahitaji maalumu.

    Alisema sababu mojawapo inayosababisha changamoto kwa watoto ni migogoro ya mara kwa mara kwa baadhi ya wanandoa ambayo ina athari hasi kwa watoto na wakati mwingine kutofanya vizuri kitaaluma na hivyo uwepo wa wataalamu wa ustawi wa jamii utasaidia kuwapa ushauri watoto ili wawe sawa kiakili.

    Tanzania imesaini  mikataba mbalimbali ya kimataifa ya watu wenye ulemavu  ikiwemo mkataba wa haki za mtoto, CRC mwaka 1989 ambapo mataifa yalikubaliana kuwa na sheria na kanuni za kulinda haki za watoto kwa mataifa wanachama.

    Sehemu ya washiriki wa kikao cha tathmini  ya kutekeleza program za kuwasaidia watu wenye ulemavu kikiwahusisha wadau mbalimbali wakiwemo, wahadhiri, walimu, maofisa maendeleo ya jamii na wafadhili kutoka nchini Norway iliyofanyika jijini Dar es salaam hivi karibuni katika ukumbi wa chuo hicho.

  • Na Grace Mwakalinga, Dar es salaam

    Serikali imetakiwa kuajiri maofisa ustawi wa jamii kwenye  shule  za  msingi jumuishi  ili kuwahudumia kikamilifu watoto wenye mahitaji maalum ambao wakati mwingine hukosa  mtu wa karibu kujua mahitaji yao wawapo shuleni.

    Mapendekezo hayo yametolewa na Mkuu wa Idara ya Ustawi wa Jamii, Chuo Kikuu Huria cha Tanzania Dkt. Mariana Makuu wakati wa kikao cha tathmini  ya kutekeleza program za kuwasaidia watu wenye ulemavu kikiwahusisha wadau mbalimbali wakiwemo, wahadhiri, walimu, maofisa maendeleo ya jamii na wafadhili kutoka nchini Norway iliyofanyika jijini Dar es salaam hivi karibuni katika ukumbi wa chuo hicho.

    Alisema mahitaji ya matunzo kwa  watoto wenye mahitaji maalumu kwenye jamii na waliopo shuleni ni makubwa kutokana na kukithiri kwa vitendo vya ukatili wa kijinsia hivyo kuna uhitaji wa walimu kuongezewa nguvu kutoka kwa maofisa ustawi wa jamii ambao watafanya kazi pamoja na walimu hao ili kuhahikisha ustawi wa watoto katika mazingira ya shule na jamii kwa ujumla.

    “Walimu peke yao hawawezi kwani wana majukumu ya  kutoa elimu lakini hili la kuwasaidia kwa mambo mengine linaweza kufanyiwa kazi na maafisa ustawi wa jamii”, alisema Dtk. Makuu.

    Alisema kutokana na changamoto hiyo Chuo Kikuu Huria cha Tanzania kinaishauri serikali kuajiri maofisa ustawi wa jamii kwenye shule zote jumuishi ili kuongeza nguvu ya kuwasaidia watoto hao kielimu, kiakili na kiafya ili  wawe sawa kama watoto wengine.

    “Idadi kubwa ya watoto wenye mahitaji maalum shuleni wanashindwa kutimiza ndoto zao kutokana na kukosa uangalizi maalum ili kusoma vizuri kama watoto wengine, alisema Dkt.Makuu.

    Mwalimu wa shule ya msingi jumuishi ya Uhuru Mchanganyiko, Catherine Chitanda, alisema utaratibu huo  utakuwa mwarobaini wa kuwasaidia watoto wenye mahitaji maalum shuleni kwa kupata usaidizi wa karibu kutoka kwa maofisa hao ambao watakuwepo shuleni kuwahudumia.

    Aidha Catherine alisema katika kufanikisha hilo, lazima serikali ikubali kushirikiana na jamii, walimu na maafisa ustawi wa jamii  ili kutimiza kikamilifu jukumu la  kuwatunza  watoto wenye mahitaji maalum shuleni.

    Mtalaam wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (ICT) Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, Stella Shayo, alisema katika kutekeleza programu hiyo chuo kimejipanga kutoa elimu juu ya ukatili wa kijinsia kwa wazazi, walezi na jamii juu ya athari za vitendo hivyo ili kuwaweka sawa kisaikolojia watoto hao wawapo shuleni.

    Kwa upande wake, Afisa Maendeleo ya Jamii Kata ya Kinondoni, Silider Ussuma alisema anaunga mkono jambo hilo na kwamba litasaidia kuwaweka sawa kiakili watoto wenye mahitaji maalumu.

    Alisema sababu mojawapo inayosababisha changamoto kwa watoto ni migogoro ya mara kwa mara kwa baadhi ya wanandoa ambayo ina athari hasi kwa watoto na wakati mwingine kutofanya vizuri kitaaluma na hivyo uwepo wa maafisa ustawi utasaidia kuwapa ushauri watoto ili wawe sawa kiakili.

    Tanzania imesaini  mikataba mbalimbali ya kimataifa ya watu wenye ulemavu  ikiwemo mkataba wa haki za mtoto, CRC mwaka 1989 ambapo mataifa yalikubaliana kuwa na sheria na kanuni za kulinda haki za watoto kwa mataifa wanachama.

  • Na Slyvester Richard, Singida

    Mahakama ya Wilaya Singida imemuhukumu Baraka Joel ambaye pia anajulikana kwa jina la Yohana (23), mkulima na mkazi wa Mughamo Manispaa ya Singida kwenda jela miaka 30 kwa kosa la kubaka.

    Mshitakiwa Baraka alitenda kosa hilo Februari 17, 2023 huko Mtaa na Kata ya Mughamo, Tarafa ya Ilongero, Wilaya na Mkoa wa Singida ambapo alimbaka mwanafunzi wa darasa la 7 mwenye umri wa miaka 14.

    Baada ya kutenda kosa hilo, Mshitakiwa alikamatwa na Jeshi la Polisi na kufikishwa mahakamani Machi 8, 2023 na kesi kusikilizwa na pande zote mbili.
    Kutokana na ushahidi uliowasilishwa na upande wa mlalamikaji, ulithibitisha mshitakiwa alitenda kosa hilo hivyo Mahakama kutoa adhabu hiyo Machi 14, 2024 mbele ya Mh. Hakimu Robert Uguda.

  • Na Vincent Mpepo, OUT

    Jamii imetakiwa kuasili watoto wanaoishi na kutunzwa kwenye vituo mbalimbali ili wawe sehemu ya familia hivyo kupata malezi na uangalizi unaostahili kama wanajamii wengine.

    Wito huo umtolewa na Afisa Ustawi wa Jamii, Malezi na Familia wa Jiji la Arusha, Nivoneia Kikaho wakati wa uzinduzi wa chama cha waandishi wa habari wanawake mkoa wa Arusha ‘ARUSHA WOMEN IN MEDIA’ uliofanyika mwishoni mwa wiki na kuhudhuliwa na wanawake waandishi wa mkoa huo, wanafunzi wanawake wa tasnia hiyo na wadao mbalimbali wa maendeleo.

    Alisema baadhi ya vigezo vinavyotumika ili anayekusudia kuasili mtoto kupata kibali cha mtoto wa kulea ni pamoja na utayari, maadili, usafi na mapenzi kwa watoto na kuwa utaratibu huo ni wakisheria na una taratibu za kufuata.

    “Wanadoa wanakaribishwa kuasili watoto kwa kuwa kuna mazingira rafiki tofauti na wasio kwenye ndoa”, alisema Kikaho.

    Alisema uwezo na vigezo vivyokusudiwa ni vya msingi na vya kawaida ambavyo vitamuwezesha mtoto anayeasiliwa kupata mahitaji yake muhimu.

    Hatahivyo, alisema bado kuna mwamko mdogo wa jamii kuasili watoto jambo ambalo linahitaji uhamasishaji.

    Mwenyekiti Arusha Women in Media Jamillah Omar kuasili mtoto ni kama sadaka hivyo anayeasili hapaswi kuchagua mtoto kati wengi kwenye mahali wanapoishi ili kuzuia unyanyapaa na kuwafanya wanakosa kuasiliwa kujisikia vibaya.

    Hatahivyo, kwa uzoefu wa miaka ya hivi karibuni suala la kuasili watoto halijapata kipaumbele na jamii bado kunahitajika juhudi za makusudi kuhamasisha jamii ili ione umuhimu wa jambo hilo.

  • Na Ruth Kyelula, Mbulu DC

    Viongozi wa serikali za mitaa ikiwemo watendaji na wenyeviti wa vijiji, kata na mitaa wametakiwa kutoa ushirikiano kwa shirika la UCRT linalotekeleza mradi wa mpango wa matumizi bora ya ardhi vijinini.

    Hayo yalisemwa na Katibu Tawala wa Wilaya ya Mbulu, Paulo Bura kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Mbulu Veronica Kessy wakati akifungua kikao cha uzinduzi wa awamu ya pili ya mradi wa mpango wa matumizi bora ya ardhi kwa vijiji sita chini ya Ujamaa Community Resource Team (UCRT), uliofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya wilaya ya Mbulu Machi 19, 2024.

    Alisema viongozi hao wanatakiwa kutoa ushirikiano watekelezaji wa mradi huo ili kile walichokuja nacho kiweze kuwanufaisha wananchi wa wilaya hiyo na kutimiza malengo hayo yenye nia njema.

    “Lakini sisi tulioingia kwenye awamu hii vijiji hivi sita, pia tujue sisi ni wa mfano na tunatakiwa tufanye vizuri ili kuwapa moyo wafadhili kuendelea na mradi huu kwa vijiji vingine”, alisema Bura.

    Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Hamashauri ya Wilaya ya Mbulu, Petro Tarimo aliwaomba wanufaika wa mradi wa zamani na  wapya waendelee kutoa ushirikiano kwa UCRT na kutoa elimu kwa wanchi wengine ili kuepuka migogoro ya mipaka.

     Mratibu wa Ujamaa Community Resource Team (UCRT), Dismas Meitaya ameushukuru uongozi wa Wilaya Mbulu kwa ujumla kwa ushirikiano wanaoutoa kwa takribani miaka 20 hivyo kuwawezesha kutekeleza mradi huo kwa ufaninsi.

    Malengo ya UCRT ni kuwezesha jamii ya asili kumiliki, kusimamia na kunufaika na ardhi, alisema Meitaya

    Alisema wamelenga aidi kwenye jamii ya wakusanya matunda, ambao ni wa hadzabe na waakie, wamaasai, wadatoga pamoja na wafugaji , wakulima wabatemi  na wa iraqw.

    “Huu mpango ni shirikishi sana, akina mama wanapewa kipaumbele ili washiriki kikamilifu na zaidi kuona jamii na akina mama kupitia vikundi vyao wakiwa mstari wa mbele.

    Alibainisha vijiji lengwa sita vya mradi katika bonde la Yaeda na Ziwa Eyasi ni Garbabi, Yaedakati, Dirim, Endalat, Murkuchida na Endamilay.

  • Na Mwandishi Wetu

    Sehemu ya washiriki wa hafla ya uzinduzi wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Mkoani Arusha ‘Arusha Women in Media’ katika picha za pamoja katika ukumbi na viwanja vya Jumuiya ya Afrika Mashariki iliyofanyika hivi karibuni.

    Waandishi wa habari wanawake mkoa wa Arusha wametakiwa kuchangamkia fursa kwa kujiunga na chama cha waandishi wananawake mkoani humo ili kuwa na umoja wenye nguvu na sauti moja katika kujikomboa kiuchumi.

    Mkurugenzi wa kampuni ya utalii ya Off we Go safaris Ltd Genevive Mollel ametoa wito huo wakati wa uzinduzi wa chama cha waandishi wa habari wanawake mkoa wa Arusha kijulikanacho kwa jina la ‘ARUSHA WOMEN IN MEDIA’ ulifanyika jijini Arusha na kuhudhuliwa na wanawake waandishi wa mkoa huo, wanafunzi wanawake wa tasnia hiyo na wadao mbalimbali.

    Alisema uandishi wa habari ni tasnia mtambuka ambayo yenye fursa nyingi zikiwemo za kiuchumi na kijamii hivyo waandishi wa habari waache kujifungia sehemu moja ili kuona fursa katika maeneo mengine ili waweze kujikwamua kiuchumi na kuacha utegemezi.

    Mwenyekiti Arusha Women in Media Jamillah Omar amesema lengo umoja huo ni kutumia fursa mbalimbali zitolewazo na serikali, wakala wa serikali, makampuni na taasisi mbalimbali ndani na nje ya nchi kwa ajili ya wanawake ikiwemo mikopo  yenye masharti nafuu na isiyo na riba.

    Alisema waandishi wa habari wanawake kama walivyo wanawake wengine wanakabiliwa na changamoto ya kipato kutokana na majukukumu ya familia hivyo umoja huo utawasaidia kuzifikia fursa hizo kwa pamoja na hatimae kujikwamua kimaisha.

    “Waandishi wenzangu hasa wanawake mnatambua namna ambavyo mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan amejipambanua kuwawezesha wanawake kiuchumi hivyo na sisi tujiongeze tutumie fursa hizo tuwe na vyanzo mbadala vya kujiongezea kipato”alisema Jamillah.

    Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Arusha Cloud Gwandu aliwataka waandishi wa habari wanawake kujiunga na umoja huo ili wawe na sauti moja itakayosaidia kufikia malengo yao.

    Alisema waandishi wa habari wengi sasa hivi wanapitia changamoto ya ajira ambapo asilimia kubwa hawana ajira wala mikataba ya kazi jambo ambalo ni hatari kwa ustawi wa maisha yao.

    “Tasnia ya habari kwa sasa inapitia wakati mgumu kwa kuwa kazi nyingi za serikali zimekuwa zikifanywa na maafisa habari wa serikali badala ya kutumia waandishi wa habari”, alisema Gwandu.

    Wakati huo huo Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, Vincent Mpepo aliwakumbusha waandishi kuzingtia maadili na weledi katika kazi zao na kwa kuzingatia mabadiliko ya teknolojia amabyo yana changamoto kadha wa kadha.

    Meneja wa Benki ya CRDB Tawi la Arusha, Amulikiwa Massawe alisema uzinduzi wa umoja huo umekuja wakati mwafaka ambapo benki ya CRDB  imetenga fedha nyingi kwa ajili ya kuwakopesha wanawake kwa masharti nafuu .

    “Habari njema kwa sasa ni kwamba CRDB ina akaunti maalum kwa ajili ya wanawake ikiwemo akaunti za Malkia na Imbeju ambazo zina masharti nafuu”, alisema Massawe.

    Kwa mujibu wa matokeo ya tafiti mbalimbali zilizofanyika barani Afrika na nchini Tanzania zinabainisha changamoto mbalimbali zinazoikabili tasnia ya habari ikiwemo kuyumba kiuchumi kwa vyombo vingi vya habari hivyo kushindwa kuwapa waandishi wa habari stahiki zao kwa muda muafaka ikiwemo mishahara na mikataba ya ajira za uhakika hivyo kuwafanya waendelee kuwa tegemezi jambo linaothiri pia misingi ya uandishi wa habari ambapo kuna wakati waandhi wa habari wanakuwa wasemaji wa watu badala ya umma.

  • Waandishi wa Habari wanawake wameshauriwa kuungana na kutumia fursa mbalimbali zinazotolewa na serikali ili waweze kujikwamua kiuchumi jambo ambalo litawasaidia kuwa na kipato mbadala na kuondokana na utegemezi wa kazi moja.

    Mwenyekiti wa umoja wa waandishi wa Habari mkoa wa Arusha Jamillah Omar ametoa wito huo wakati wa uzinduzi wa chama hicho cha ARUSHA WOMEN IN MEDIA ulioenda sambamba na semina elekezi iliyohusisha masuala ya ujasiriamali na fursa za mikopo zitolewazo na benki ya CRDB,Usalama wa mitandaoni kwa wanawake mada iliyotolewa na TCRA,maadili ya uandishi wa Habari na malezi bora ya Watoto.

    Jamilah amesema serikali chini ya mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan imetoa Fursa nyingi za kuwawezesha wanawake ikiwemo mikopo isiyokuwa na riba hivyo imefika wakati sasa kwa waandishi wa Habari wanawake nao kutumia fursa hiyo kujiingiza katika ujasiriamali ili waweze kuwa na chanzo kingine cha mapato.

    Amesema kutokana na kupanda kwa gharama za Maisha na mara nyingi wanawake ndio wamekuwa kukabiliwa na majukumu mengi ya malezi ya familia wamekuwa wakikumbana na changamoto ya kipato hivyo wakati mwingine kusababisha kuzidiwa na majukumu ambapo kwa kutumia fursa ya umoja huo itawasaidia kuungana na kunufaika na fursa mbalimbali.

    “Siku zote sisi kama waandishi wa Habari tumekuwa vianara wa kuripoti matukio mbaimbali ikiwemo hizi fursa za mikopo kama ya Halmashauri inayotolewa kwa ajili ya wanawake vijana na watu wenye ulemavu lakini sisi kama waandishi wa Habari wanawake tumetumia vipi fursa hiyo?alihoji Jamillah

    “Imefika wakati sasa waandishi wa Habari wanawake tubadilike kwanza tumechelewa sana kila mtu anatushangaa tulikuwa wapi hadi leo hatuna umoja wa kama huu”alisema

    Mgeni Rasmi katika hafla hiyo mfanyabiashara mjasiriamali wa sekta ya utalii Genevive Mollel amewapongeza waandishi wa Habari wanawake mkoa wa Arusha kwa kuanzisha umoja huo ambapo amewatoa hofu kuwa ujasiriamali si kitu kigumu na kusisitiza kuwa wanaweza kutokana na tasnia na uwanda mpana katika kila sekta.

    “katika sekta yenu ya Media inafursa nyingi sana mnakutana na watu wengi sana kila siku kila mahali kwa mfano kwenye sekta ya utalii hatuwezi kupanda bila media kuna vivutio vingi ambavyo vinatanganzwa kwa kupitia media hii ni fursa”alisema Genevive

    Awali mwenyekiti wa klabu ya waandishi wa Habari mkoa wa Arusha Cloud Gwandu akizungumza katika hafla hiyo amewapongeza waandishi wa Habari wanawake kwa kuungana na kusema kuwa dunia ya sasa bila kuungana huwezi kufanya kitu chochote kikubwa hata kama unakili au uwezo kama nani.

    “Ninawaomba waandishi wa Habari ambao hawajajiunga kujiunga na chama hicho ili kiwe na nguvu ili wawe na sauti moja itakayosikika itakayowasaidia kuwafikisha mbali”alisema Gwandu

    Amesema hivi sasa tasnia ya uandishi wa Habari inakabiliwa na changamoto kubwa ya kazi zao nyingi kufanywa na maafisa Habari wa serikali jambo ambalo limepunguza wigo wa waandishi kupata kazi za kufanya hivyo kwa umoja huo itawasaidia kubadilishana Mawazo na kutumia vyema fursa mbadala kujikwamua kiuchumi.

    Gwandu amesema waandishi wengi wa Habari hawana ajira hivyo uhakika wa kipato chao ni mdogo hali inayowazalimu wakati mwingine kuwa omba omba kwa wadau hali ambayo amesema imekuwa ikiwadhalilisha.

  • By Vincent Mpepo, OUT

    The Eastern Africa Regional Early Childhood Conference will start on 11th to 14th Mach, 2024 at Julius Nyerere International Convention Centre in Dar es Salaam and will involve participants from Tanzania and outside Tanzania.

    According to the information from the organizers’ website, this years’ conference theme is ‘Investing in Early Childhood: Building Human Capital along the Life Course’ and it will be open to multisectoral stakeholders interested in improving early childhood outcomes.

    “Policy Makers, CSOs/FBOs/CBOs, Grassroots Advocacy Organizations including Women and Youth Groups, Academia and Development Partner Organizations”, says part of the information from the website.

    The conference will provide an opportunity for stakeholders and participants to take stock of the status of early childhood in the sub region, showcase innovative programs in the sub-region, foster dialogue that promotes knowledge exchange and learning and build consensus around key advocacy issues.

    The conference presentations will be an in-person with different sessions to ensure wide and active participation and provide avenues for generating insights that will be taken up in the conference recommendations, final communication and plans for action.

    The conference will employ plenary sessions where keynote presentations will be made along with panel sessions that spotlight country experiences, oral paper presentations in thematic break-out parallel sessions, round table discussions for smaller groups that allow for in-depth engagement and learning sessions.

    Moreover, other presentation modalities are not limited to side events to support capacity building and joint planning for various interest groups.

    These presentation modalities will enable groups to engage, network and build pathways for collaboration and partnerships that would take Early Childhood forward in the region and lastly exhibition of partner initiatives and sharing of materials and resources.

    According to Dr. Evangeline Nderu, the conference is expected to receive participants from Kenya, Uganda, Rwanda, South Sudan, Mozambique; South Africa and from outside Africa.

    For more information visit: https://afecn.org/2024ear-conference

    Group photos of rapporteurs which include students and a lecturer from the Aga Khan University during the orientation before the start of the conference. (Picture by Vincent Mpepo).

  • Na Vincent Mpepo, Dar es salaam

  • Na Vincent Mpepo, OUT

    IMEELEZWA kuwa baadhi ya sheria, taratibu na kanuni za manunuzi nchini ni kikwazo kinachokwamisha utelekezaji wa miradi kwa muda uliopangwa na kusababisha wananchi kutopata huduma kwa muda uliopangwa.

    Hayo yamebainishwa na Mratibu Mkuu wa Mradi wa Mageuzi ya kiuchumi, Profesa Deus Ngaruko katika siku ya pili ya kikao kazi cha siku tatu kinachoendelea Mkoani Pwani Wilaya ya Bagamoyo na kuhusisha waratibu wa mradi katika idara zote na wakurugenzi wa vituo vya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania ambao mradi huo unatekelezwa katika vituo vya mikoa wanavyovisimamia.

    Alisema taratibu, kanuni na sheria za manunuzi zinaleta ugumu katika kutekeleza masuala mbalimbali ikiwemo miradi wa mageuzi ya kiuchumi unaofadhiliwa na Benki ya Dunia.

    “Fedha zipo lakini tunashindwa kuzitumia kutekeleza mradi kwa wakati kwa sababu kuna taratibu ambazo zinatumia muda mrefu kukamilika, kuna haja kuangaliwa kwa taratibu hizi,”alisema Profesa Ngaruko.

    Mratibu wa uhuishaji mitaala, Dkt. Halima Kilungu alisema utekelezaji wa miradi kama huu wa mageuzi ya kiuchumi unahitaji wafanyakazi wa taasisi husika kutoka idara na vitengo vyote kushirikiana ili kuhakikisha kuwa changamoto za ndani zinatatuliwa ili kwa pamoja kuhakiksha mradi unatekelezeka kwa faida ya taasisi na taifa kwa ujumla.

    “Ni muhimu kwa wafanyakazi wa idara zote ndani ya taasisi kushirikiana ili kuhakikisha kuwa mradi unafanikiwa kwani ukifeli ni taasisi na taifa limefeli”, alisema Dkt.Kilungu.

    Kwa upande wake, Mratibu wa Manunuzi wa Mageuzi ya kiuchumi chuoni hapo, Daudi Sospeter alisema ni muhimu kufuata taratibu, sheria na kanuni za manunuzi ili kuondokana na changamoto za kiuhasibu na mahesabu.

    “Sheria za manunuzi zinaweza kuwa na tasfiri tofauti na ilivyokusudiwa”, alisema Sospeter.

    Alisema lengo la kusimamia sheria, kanuni na taratibu za manunuzi ili yaende kwenye mamlaka husika

    Mradi wa mageuzi ya kiuchumi wa miaka mitano kupitia ufadhili wa Benki ya Dunia una lengo la kukuza elimu ya juu kama chachu ya uchumi mpya wa Tanzania ikihusisha kupanua uwezo wa vyuo vikuu katika maeneo muhimu ya uvumbuzi, kuongeza soko la ajira na kwa kuwekeza katika miundombinu inayohitajika kwa ufundishaji na utafiti wa kisasa.