
Na Mwandishi Wetu
Spika wa Bunge la Australia, Milton Dick, amechaguliwa kuwa Rais mpya wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), akimrithi Dk. Tulia Ackson, aliyemaliza muda wake. Dick anatarajiwa kuiongoza taasisi hiyo kwa kipindi cha mwaka 2026 hadi 2029.
Dick ameshinda uchaguzi huo kwa kura 182, sawa na asilimia 56 ya kura zote zilizopigwa na wajumbe wa Mkutano wa 153 wa IPU, unaoendelea jijini Arusha.
Katika uchaguzi huo, Dick aliwashinda Spika wa Bunge la Milli Majlis la Azerbaijan, Prof. Dk. Sahiba Gafarova, aliyepata kura 124, sawa na asilimia 38, pamoja na Seneta wa Chile, Rojo Edwards, aliyepata kura 21, sawa na asilimia sita.
Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo leo, Oktoba 9, 2026, Dk. Tulia Ackson amesema Dick ndiye mshindi wa uchaguzi wa urais wa IPU kwa kipindi cha mwaka 2026 hadi 2029.
Akizungumza baada ya kuchaguliwa, Dick amesema anaipokea nafasi hiyo kwa unyenyekevu na shukrani, akieleza kuwa ni heshima kubwa zaidi katika maisha yake.
Leave a Reply